loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Uwekezaji zaidi wahitajika sekta ya sukari

SEKTA ya sukari nchini inahitaji kasi kubwa ya uwekezaji kutokana na mahitaji makubwa ya sukari, ikilinganishwa na kiasi kinachozalishwa kwa sasa, imebainika.

Waziri wa Kilimo, Japhet Hasunga alisema hayo katika maadhimisho ya Siku ya Mkulima, yaliyofanyika Kituo cha Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Kibaha (Tari Kibaha) mkoani Pwani.

Hasunga alisema msimu wa mwaka 2020/2021, serikali imeweka mikakati madhubuti ya kuhakikisha nchi inajitosheleza kwa sukari, ikiwamo kuviagiza viwanda vyote vya sukari nchini kuongeza uzalishaji wao ili kukidhi mahitaji makubwa yaliyopo nchini.

Kwa maelezo ya Hasunga, mahitaji ya sukari nchini yamekuwa yakibadilika mwaka hadi mwaka kulingana na hali ya mahitaji kwa mwaka husika. Hivyo, serikali imeweka mikakati ya kuongeza uzalishaji wa sukari kwa kuzingatia fursa zilizopo, ikiwemo ardhi nzuri na mahitaji makubwa ya soko hususan la ndani.

“Mikakati hiyo ni pamoja na kuhamasisha uwekezaji wa mitaji katika sekta ya sukari nchini kwa kuanzisha miradi mbalimbali ya uzalishaji wa sukari.

“Miradi hiyo ni pamoja na Mkulazi 1 na Mkulazi 11 mkoani Morogoro, uanzishwaji wa viwanda vya sukari katika maeneo mbalimbali nchini yakiwemo Chamwino mkoani Dodoma, Geita, Kasulu mkoani Kigoma, Rufiji mkoani Pwani, Songea mkoani Ruvuma na Bagamoyo mkoani Pwani,” alisema.

Mkurugenzi Mkuu wa Tari, Dk Geoffrey Mkamilo alisema taasisi hiyo inasimamia utafiti, inahamasisha matumzi ya teknolojia pamoja na shughuli za utafiti, hivyo kituo hicho cha Kibaha shughuli yake kubwa ni utafiti wa miwa.

“Tumia teknolojia za kilimo na utawala bora kwa ukuaji wa ...

foto
Mwandishi: Lucy Ngowi

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi