loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Washiriki Sabasaba wajihadhari corona

MAONESHO ya 44 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (DITF) maarufu Sabasaba, yameanza kwa waandaaji Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade), kuhakikisha kila mshiriki anaweka chombo cha kunawia mikono, kama njia mojawapo ya kujilinda na maambukizi ya virusi vya corona.

Aidha, kila mlango wa kuingilia kwenye viwanja vya maonesho hayo kwenye Viwanja vya Mwalimu Nyerere Barabara ya Kilwa, Temeke, vimewekwa vyombo vya kunawia mikono na kuna Kamati ya Afya ambayo inafuatilia hali ilivyo katika kuhakikisha maonesho hayo yanafanywa katika hali ya usalama.

Akizungumzia kuanza kwa maonesho hayo jana, Naibu Mkurugenzi Mkuu wa TanTrade, Lafita Khamis alisema maonesho hayo yataendelea hadi Julai 13, mwaka huu na yanatoa fursa kwa washiriki kuona fursa mbali mbali, ikiwemo kupata masoko na bidhaa zao ndani na nje ya nchi.

Khamis alisema wamezingatia masuala ya usalama wa afya kwa washiriki, kwa kila milango wa kuingilia kwenye maonesho hayo kuna vyombo vya kunawia mikono na pia kila banda la washiriki nako kuna vyombo vya kunawia, kabla ya kuingia ili kuepuka uwezekano wa kupata maambukizi ya virusi vya corona.

Alisema leo kutakuwa na mikutano miwili ya ana kwa ana ya wafanyabiashara maarufu kama (B2B) ambayo itaendeshwa kwa njia ya mtandao na itahusu sekta ya matunda na mbogamboga, na ile ya viungo.

Mmoja wa washiriki, Michael Joseph alisema walianza kuandaa banda jana na leo asubuhi watalikamilisha na kupanga bidhaa.

Alisema maonesho hayo yamepoa kutokana na washiriki wengi wa nje kutoshiriki.

KATIBU Tawala Mkoa wa Kagera, Profesa Faustine Kamuzora, amewaomba wamiliki ...

foto
Mwandishi: Ikunda Erick

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi