loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Msajili ataka vyama vijikosoe

OFISI ya Msajili wa Vyama vya Siasa imevitaka vyama hivyo kujikosoa na kuhakikisha vinaingia kwenye uchaguzi mkuu bila ‘makandokando’ ya aina yoyote.

Naibu Msajili wa Vyama vya Siasa, Mohamed Ali Ahmed alitoa rai hiyo juzi jijini Dar es Salaam wakati wa kufunga kikao kati ya ofisi yake na viongozi wakuu wa vyama 19.

Alihimiza vyama vyote kufanya uchaguzi kwa amani na utulivu vikiwa vimerekebisha kasoro vilivyo nazo. Alitaka vijipange kwenye uchaguzi vikiwa imara kuleta ushindani, badala ya kuwa wasindikizaji.

“Vyama vinatakiwa viwe imara, vijisafishe, vijikosoe wakati vikielekea kwenye uchaguzi mkuu. Tuingie kwenye uchaguzi tukiwa safi, tuna nguvu, tuna uwezo na tumeondosha makandokando yote tuliyo nayo,” alisema.

Ahmed alisisitiza kuwa raha ya ofisi ya msajili ni kuona vyama vinakuwa na nguvu.

Aliwataka viongozi wa vyama kuwa wavumilivu wa kisiasa na kushindana kwa hoja kwa ajili ya maendeleo ya nchi.

Akiwahimiza kupiga vita ubaguzi wa dini, jinsia na kabila, naibu msajili alisema mafunzo waliyopata kupitia kikao hicho ni hatua moja kuelekea kwenye uchaguzi ulio huru, salama na amani.

Alisema ofisi yake inachukulia vyama vyote ni sawa, kwa maana kwamba hakuna kikubwa wala kidogo.

“Vyote vina haki sawa na vinastahili kupata mafunzo, kujengewa uwezo ili kushinda uchaguzi mkuu,” alisema.

Kikao hicho kilichofunguliwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu), Jenista Mhagama, kilihusisha wenyeviti wa taifa, makatibu wakuu na wanachama wanaohusika na masuala ya sheria wa vyama hivyo vya siasa.

Wagombea kutoka vyama vya ...

foto
Mwandishi: Stella Nyemenohi

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi