loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

UDOM kuwezesha wanataaluma wachanga

MKUU wa Ndaki ya Biashara na Sheria katika Chuo Kikuu cha Dodoma, Profesa Adam Mwakalobo amesema chuo hicho kimetenga fungu maalumu kwa ajili ya kuwasaidia wanataaluma wachanga wanaochipukia.

Profesa Mwakalobo ameyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari baada ya kufungua mafunzo ya uhuru wa kujieleza kwa wanataaluma.

Amesema chuo kimetenga fungu maalumu kwa ajili ya kuweza kuwasaidia wanataaluma wachanga wanaochipukia.

“Chuo kinawasadia wanataaluma wachanga waweze kuomba zile fedha yaani ni mashindano na wakipata wanaenda kufanya tafiti mbalimbali kulingana na maeneo yao ingawa sio kitu kikubwa sana lakini ni kuwawezesha ili waweze kujiendeleza kwa sababu unajua kuandika machapisho na kwenda kushindana ni lazima uwe umejifunza namna ya kuandika andiko,” amesema Profesa Mwakalobo.

Alisema mafunzo yatakuwa ni endelevu kwa sababu mwalimu muda wote anapaswa kupata mbinu mpya na vitu vipya kwani kila siku kumekuwa na mabadiliko mapya.

“Unajua mabadiliko yapo kila siku na kuna vitu ambavyo vinaingia kwa hiyo ni lazima tupate mbinu mpya za kufundisha na kujifunza huwezi kukaa tu muda wote lazima upate mbinu mpya za kufundisha uongeze ujuzi kila wakati kwa sababu ya haya mabadiliko yanayoendelea ndiyo maana ya haya mafunzo,” alisema.

Alisema wanataaluma wanatakiwa kuwa na uhuru wa kuchapisha kulingana na mambo wanayoyaona, machapisho ni moja kati ya vigezo vinavyotakiwa kutimizwa ili wapande vyeo.

Mkuu wa Idara ya Sheria Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), Dk Ines Kajiru alisema mafunzo kama hayo yamekuwa yakifanyika ili kukuza uelewa na kuwasaidia wanataaluma kuwajengea uwezo katika masuala mbali mbali.

“Ni wengi wanaonufaika katika mafunzo kama haya, nitolee mfano hapa leo watakaonufaika ni walimu wanataaluma wote wa Ndaki ya Taaluma za Biashara na Sheria wa Chuo Kikuu cha Dodoma,” alisema Kajiru.

“Tunacholenga ni kuendelea kukuza uelewa na kuwasaidia wanataaluma kuwajengea uwezo zaidi wa mambo mbalimbali kuhusu elimu na vilevile uhuru wa kujieleza na uhuru wa elimu,” alisema.

Mwalimu katika Shule ya Sheria, Nicodemus Kusenha ambaye pia ni Katibu wa Mtandao wa Kliniki za Sheria katika Vyuo Vikuu Afrika Mashariki (EANUUALAC), alisema mafunzo kama hayo yanaongeza uelewa juu ya dhana nzima ya uhuru wa kujieleza.

MWITO umetolewa kwa wakulima kwenye mikoa yanayozalisha chakula kwa wingi ...

foto
Mwandishi: Sifa Lubasi, Dodoma

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi