loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Takukuru yaokoa mil 310/- Dodoma

TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) mkoani Dodoma imeokoa jumla ya Sh milioni 310.1 zikiwemo fedha zilizolipwa kwa wakandarasi kinyume cha utaratibu na fedha zilizofujwa na wasimamizi wa miradi.

Katika mkutano wake na waandishi wa habari jana, Mkuu wa Takukuru Mkoa, Sosthenes Kibwengo alisema katika kipindi cha Aprili hadi Juni mwaka huu, ufuatiliaji kwa njia ya uchunguzi na udhibiti umewezesha kuokoa garo moja, mashamba 13 yenye jumla ya ekari 30, viwanja viili, nyumba mbili, vitambulisho 375 vya wajasiriamali na jumla ya Sh milioni 310.1.

Alisema fedha zilizookolewa zimetokana na ukusanyaji wa madeni ya vyama vya akiba na mikopo (Saccos), fedha za vitambulisho vya wajasiriamali ambazo hazikuwa zimewasilishwa, fedha zilizolipwa kwa wakandarasi kinyume na utaratibu, fedha zilizofujwa na wasimamizi wa miradi, fedha za kodi ya zuio na matazamio zilizochepushwa.

Pia alisema fedha zaa mikopo umiza, viwanja vilivyouzwa bila kufuata utaratibu, faini na kuchelewa kukamilisha miradi, mashamba na nyumba zilirejeshwa na wananchi wanyonge ambao walidhulumiwa na wakopeshaji wasiozingatia taratibu za ukopeshaji.

Aidha, taasisi hiyo imemfikisha mahakamani aliyekuwa Kaimu Katibu wa Tume ya Utumishi wa Walimu Wilaya ya Bahi, Adam Richard (49) kwa makosa manane ya kuomba na kupokea rushwa ya Sh 450,000.

Mkuu huyo wa Takukuru alisema Richard alifunguliwa shauri la jinai la kuomba rushwa, akishtakiwa kwa makosa manane ya kuomba na kupokea rushwa ya Sh 450,000 kutoka kwa walimu wawili ili awasaidie katika mchakato wa kupandishwa madaraja.

Alisema pia mshitakiwa huyo Machi 25, mwaka huu alifikishwa mahakamani na kufunguliwa mashauri manne kuhusu rushwa na uchunguzi dhidi yake unaendelea kwani inaonesha alichukua fedha kutoka kwa walimu wengi.

Aidha, alisema taasisi hiyo kwa robo ya Aprili hadi Juni mwaka huu, imejikita katika eneo la kuzuia na kupambana na rushwa kulingana na majukumu yake.

Alisema katika kipindi hicho fursa mbali mbali zilipatikana katika kuelimisha nanchi kuvunjwa ukimya na kutoa taarifa za vitendo vya rushwa ya ngono.

“Pamoja na suala la rushwa ya ngono msisitizo mingine ulikuwa ni kwenye uelimishaji katika kipindi hiki kuelekea uchaguzi ambapo wananchi walielimishwa juu ya makosa ya rushwa kwenye chaguzi na madhara yake, thamani ya kura na wajibu wa kushiriki kivitendo katika kuzuia rushwa katika uchaguzi,” alisema.

MWITO umetolewa kwa wakulima kwenye mikoa yanayozalisha chakula kwa wingi ...

foto
Mwandishi: Sifa Lubasi, Dodoma

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi