loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Simba yaifuata Yanga FA

SIMBA imeifuata kibabe Yanga baada ya kuifunga Azam FC 2-0 kwa katika mchezo wa robo fainali ya Kombe la Shirikisho uliofanyika kwenye Uwanja wa Taiifa, jijini Dar es Salaam jana.

Mabao ya Simba yaliyofungwa na John Bocco na Clatous Chama na hivyo kutinga kwa kishindo katika nusu fainali ya michuano hiyo.

Kwa ushindi huo, Simba sasa watakutana na Yanga katika nusu fainali ya kombe hilo, ambalo pia linajulikana kama Azam Federation Cup.

Mbali na kutinga nusu fainali, kipigo hicho kimeivua pia Azam ubingwa wa taji hilo, ambalo liliiwezesha timu hiyo msimu uliopita kushiriki Kombe la Shirikisho la Afrika.

Yanga wenyewe walipata nafasi hiyo baada ya juzi kuifunga Kagera Sugar 2-1 kwenye Uwanja wa Taifa.

Wakati huohuo, Simba itakabidhiwa taji lao la Ligi Kuu Tanzania Bara Julai 8 baada ya mchezo wake wa ligi hiyo dhidi ya Namungo utakaofanyika kwenye Uwanja wa Majaliwa, Lindi.

Simba ilitangaza ubingwa baada ya kutoka suluhu na Tanzania Prisons katika mchezo uliofanyika kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya nakufikisha pointi 79, ambazo haziwezi kufikiwa na timu yoyote inayoshiriki ligi hiyo.

BAADA ya Yanga kurejea na ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi