loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

SAHARE YATINGA NUSU FAINALI FA

TIMU ya Sahare All Stars jana imefanikiwa kutinga hatua ya nusu fainali ya michuano ya Kombe la Shirikisho (FA) baada ya kuwafunga Ndanda FC kwa mikwaju ya penalti 4-3 katika mchezo uliofanyika kwenye Uwanja wa Mkwakwani Tanga .

Katika mechi hiyo iliyokuwa kali, ilifikia kwenye hatua ya matuta baada ya mechi kukamilika ndani ya dakika 90 kwa timu hizo kutoka sare ya kufungana bao 1-1 huku mabao yote ya kipatikana kipindi cha pili, ambapo wenyeji Sahare All Stars walikuwa wa kwanza kupata bao dakika ya 49 lililowekwa kimiani na Kassim Haruna wakati Ndanda walisawazisha dakika ya 53 kwa mkwaju wa penalti kupitia kwa Abdul Hamis.

Penalti za Sahare zilifungwa na Haruna, Salimu Said, Hussein Hussein na Omary Ayub wakati walioifungia Ndanda walikuwa, Abdul Mohamed, Hamis na Omary Mponda .

Waliokosa mikwaju kwa upande wa All Stars ni Hussein Said na Ndanda ni Aziz Sibo na Vitalis Mayanga, huku nyota wa mchezo wa kipa Sahare, Fikirini Bakari.

Kwa matokeo hayo, Ndanda inayoshiriki Ligi Kuu imeaga rasmi michuano hiyo wakati All Stars ya Ligi Daraja la Kwanza inaungana na timu za Yanga ,Namungo ambazo zilishajikatia tiketi kwenye michezo iliyofanyika juzi.

Ally Stars wanajipanga kuwakabili Namungo kwenye mchezo wa hatua ya nusu fainali ya kwanza wakati huo Yanga watakaocheza fainali ya pili, bado wanamsubiri mshindi atakayepatikana kati ya Simba dhidi Azam FC mchezo ambao uliotarajiwa kufanyika jana usiku kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Azam FC ndiye bingwa mtetezi na bingwa atakayepatikana katika mchezo wa fainali ya michuano hiyo itakayofanyika kwenye Uwanja wa Nelson Mandela, Sumbawanga, Rukwa.

MZUNGUKO wa nne wa Ligi Kuu soka Tanzania bara umemalizika ...

foto
Mwandishi: Tuzo Mapunda

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi