loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Klabu zaonywa kupanga matokeo

BODI ya Ligi Tanzania (TPLB) imetoa onyo kali kwa wale wote watakaopanga njama au kushiriki kupanga matokeo wakati huu Ligi Kuu, Ligi Daraja la Kwanza na la Pili zikielekea ukingoni.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo iliyotolewa Dar es Salaam jana, kanuni ya 30 ya upangaji matokeo, Bodi hiyo katika taarifa yake hiyo ilisema kuwa timu itakayopanga matokeo itafungiwa miaka 10 ya kutozwa faini ya Sh milioni 10.

Endapo timu yoyote itabainika kupanga matokeo ya mchezo wowote waliocheza itachukuliwa hatua zifuatazo: Mtu yeyote aliyekula njama na kushawishi kupanga matokeo ataadhibiwa kwa kusimamishwa kushiriki mechi na kutoshiriki shughuli yoyote ya mpira wa miguu kwa kipindi cha miaka 10 na faini isiyopungua Sh milioni 10.

Pia katika shauri linalovuruga hadhi ya mpira wa miguu, muhusika atafungiwa maisha kujishughulisha na mpira wa miguu. Ikiwa mchezaji au kiongozi atajishughulisha katika upangaji matokeo kama ilivyo katika kanuni ya 30 (1a) klabu au mkoa, ambao mchezaji au klabu inatoka utapigwa faini. Katika makosa mazito ataondolewa katika ligi, kushushwa daraja, kupunguzwa pointi na kurudisha zawadi.

BAADA ya Yanga kurejea na ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi