loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Mtibwa- Tutapambana tubaki Ligi Kuu

TIMU ya Mtibwa Sugar imejinasibu kuendelea kupambana kuhakikisha kikosi hicho kinasalia kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara msimu ujao.

Kauli hiyo ilitolewa na Ofisa Habari wa Mtibwa jana, Thobiasi Kifaru baada ya kikosi hicho kuwa katika nafasi ya 13 kwenye msimamo wa ligi hiyo wakiwa na jumla ya pointi 37 wakicheza mechi 32, huku wakisaliwa na mechi sita tu, ambazo wanatakiwa kupata ushindi ili kuendelea kubaki katika ligi hiyo.

Akizungumza kutoka Morogoro jana, Kifaru alikiri kikosi hicho kupitia katika mazingira magumu ndani ya msimu huu unaolekea ukingoni kwa kushika nafasi, ambayo hawajaizoea kuikalia, kama ilivyosasa.

“Nakiri ni msimu mgumu kwetu ambao umetufanya kubaki kwenye mazingira magumu ambayo hatujawahi kushika kwenye msimamo wa Ligi tangu tumepanda kwa kushika nafasi ya 13 kwenye msimamo hatuwezi kukata tama, bado tuna mechi sita za kupigania tubaki, ”alisema Kifaru.

Alisema katika kipindi hiki, benchi la ufundi kwa kushirikiana na viongozi wengine bado wanaendelea kutimiza majukumu yao kwa kuhakikisha vijana wa kikosi hicho wanaandaliwa kiushindani kwa michezo iliyobaki ili kupata ushindi kwa mechi zilizosalia.

Alisema licha ya kwamba wanacheza michezo hiyo, huku Simba ikiwa tayari imeshachukua ubingwa, lakini wao bado wanapresha kubwa ya kupambana kusaka pointi muhimu za kuepuka kushuka daraja msimu huu wa mwaka 2019/2020.

KOCHA Mkuu wa Simba, Didier Gomes ...

foto
Mwandishi: Tuzo Mapunda

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi