loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Cheka amwendea Phiri Milimani

BONDIA Cosmas Cheka amesema anafanya mazoezi ya milimani kujiandaa na pambano la kimataifa dhidi ya Mmalawi, Hannock Phiri litakalofanyika Morogoro Agosti mwaka huu.

Akizungumza na gazeti hili jana, Cheka alisema maandalizi yake yanakwenda vizuri na amekuwa akitumia milima ya mkoa huo kufanya mazoezi yake ya pumzi kujiweka tayari.

“Nimekuwa nikifanya mazoezi milimani, huku Morogoro kujiweka vizuri na baadaye kocha wangu akishamsoma mpinzani, atanipa mbinu za kukabiliana naye, naamini kwa uwezo wa Mungu nitafanya vizuri,”alisema.

Bondia huyo ambaye ni mdogo wake bondia mwingine, Francis Cheka alisema anataka kushinda, hivyo ni lazima afanye maandalizi mazuri yatakayomwezesha kumpiga mpinzani wake na kuweka heshima.

Alisema hamfahamu vizuri mpinzani wake kwa kuwa muda bado upo na atahakikisha anamfuatilia kabla ya kupanda ulingoni.

Cheka ni miongoni mwa mabondia wenye uzoefu ingawa jina lake limekuwa likipungua umaarufu siku za karibuni.

Amecheza mapambano 12 ya kimataifa, na kati ya hayo, ameshinda mapambano manne na kupata sare moja na kupigwa saba.

Mpinzani wake anaonekana bado hana uzoefu wa kutosha, ni mgeni akiwa amecheza mapambano mawili ya nyumbani, kwao na kushinda yote hivyo, hilo litakuwa pambano lake la kwanza la kimataifa.

foto
Mwandishi: Grace Mkojera

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi

Kila mchezaji wa kigeni mil 4

masaa 19 yaliyopita Rahel Pallangyo

KLABU ya ...

Kila mchezaji wa kigeni mil 4

masaa 19 yaliyopita Rahel Pallangyo

KLABU ya ...

Simba yamuwekea kizuizi Senzo Yanga

masaa 19 yaliyopita Mohammed Mdose

SIKU moja ...