loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Kigwangalla- Watanzania wekezeni kwenye utalii

WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Dk Hamisi Kigwangalla amewashauri Watanzania wajitokeze kuwekeza katika biashara ya utalii kwa kuwa masharti ya kuwekeza katika biashara hiyo yamerahisishwa na serikali.

Dk Kigwangalla aliyasema hayo jana jijini Dar es Salaam wakati akizindua Mkakati wa Kukuza Utalii wa Ndani unaolenga kutoa ajira na kuwahamasisha Watanzania washiriki na kuwekeza katika sekta ya utalii na kuvitembelea vivutio vya utalii vilivyopo nchini.

Alisema tangu kuingia Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais John Magufuli yamefanyika mabadiliko mbali mbali yaliyolenga kuleta tija na kuifungamanisha sekta ya utalii na maendeleo ya watu kwa kuhakikisha wananchi wananufaika na sekta hiyo.

Alisema serikali ilifanya jitihada za makusudi za kulegeza masharti na kushusha viwango vikubwa vya tozo vilivyokuwepo vilikuwa vinawazuia wafanyabiashara wadogo hasa wazawa washindwe kuingia katika sekta hiyo.

Alisema tangu kuondolewa kwa masharti hayo Watanzania wazawa wanaofanya biashara ya huduma za utalii wameongezeka kutoka 1100 hadi kufikia 2,000.

“Tumia teknolojia za kilimo na utawala bora kwa ukuaji wa ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Maalumu

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi