loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Messi afikisha bao la 700

LIONEL Messi, alifunga bao lake la 700 katika historia yake ya soka kwa penalti ya aina yake, wakati timu hiyo ikitoka sare ya 2-2 dhidi ya Atletico Madrid juzi Jumanne.

Vigogo hao wa Hispania mfungaji wao huyo anayeongoza kwa mabao wakati wote, alifunga bao hilo la 700 kwa klabu yake na nchi yake, baada ya kupiga penati kwa kuuchipu mpira taratibu na kuujazaa wavuni, huku kipa akienda upande tofauti na mwelekeo wa mpira.

Bao hilo liliifanya Barcelona kuwa mbele kwa mabao 2-1, lakini Atletico walionesha ubabe wao baada ya kurudisha bao hilo na kufanya matokeo kuwa 2-2 hadi mwisho wa mchezo huo.

Kwa matokeo hayo, Barca imeendelea kubaki katika nafasi ya pili, pointi moja nyuma ya vinara Real Madrid, ambao bado wana mchezo mmoja mkononi.

Penalti hiyo ya Messi pia ni bao lake la 630 katika mechi 724 kwa klabu hiyo. Nyota huyo wa Argentina alicheza sehemu ya mwanzo wakati wakitengeneza bao la kwanza, wakati mpira wake wa kona ulimgonga Diego Costa na kubadili mwelekeo na kujaa wavuni. Mshambuliaji wa zamani wa Chelsea, Costa alipata nafasi ya haraka kufanya mabadiliko pale Atletico ilipozawadiwa penalti baada ya Yannick Carrasco kuchezewa vibaya ndani ya boksi. Costa alipiga penalti hiyo lakiniiliokolewa na kipa wa Barca, Marc-Andre ter Stegen, kabla ya kupigwa tena kwa sababu kipa alitoka mapema kabla ya mpira kupigwa. Saul Niguez alipiga penalti ya pili na kuijaza wavuni, huku Ter Stegen akienda `sokoni’.

Messi aliifungia Barcelona na kuifanya kuwa mbele na kufikisha bao la 700, akipiga penati kwa mtindo wa Panenka, ambao ulipewa jina hilo maarufu kutokana na upigaji penati uliokuwa ukifanywa na Antonin Panenka, aliyekuwa mchezaji wa kimataifa wa Czechoslovakia katika fainali za Ulaya mwaka 1976.

Hata hivyo, Niguez alisawazisha tena kwa penati nyingine wakati Barca akipoteza pointi mbili, ambazo zinaweza kuwagharimu katika mbio zao za kutetea ubingwa wa La Liga. Kwa mujibu wa takwimu zilizopatikana, Messi sasa ni mmoja wa wachezaji saba waliofunga mabao 700 katika historia yao ya soka.

Mchezaji wa Czech na Australia, Josef Bican, ndiye anayeongoza orodha hiyo kwa kufunga mabao 805 katika historia yake ya soka, akifuatiwa na gwiji wa Brazil Romario, ambaye alifunga mabao 772, pamoja na Mbrazil mwenzake Pele anayeshika nafasi ya tatu kwa kufunga mabao 767.

Gwiji wa Hungary Ferenc Puskas, alifunga magoli 746, wakati mshambuliaji wa zamani wa Ujerumani, Gerd Muller, yuko katika tano bora baada ya kufunga mabao 735.

Mpinzani mkubwa wa Messi katika ufungaji wa mabao, Cristiano Ronaldo, mwenyewe anashikilia nafasi ya sita katika orodha hiyo, baada ya kufikisha mabao 700, akifunga wakati akiwa na timu ya taifa ya Ureno katika mechi ya kufuzu kwa Euro 2020 walipocheza dhidi ya Ukraine Oktoba mwaka jana. Aliongeza mabao mengine 26 katika orodha yake tangu wakati huo.

foto
Mwandishi: BARCELONA, Hispania

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi

Kila mchezaji wa kigeni mil 4

masaa 17 yaliyopita Rahel Pallangyo

KLABU ya ...

Kila mchezaji wa kigeni mil 4

masaa 17 yaliyopita Rahel Pallangyo

KLABU ya ...

Simba yamuwekea kizuizi Senzo Yanga

masaa 18 yaliyopita Mohammed Mdose

SIKU moja ...