loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Kampuni zilizofungwa zaaswa kusaidia wafanyakazi

NAIBU Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana na Ajira), Antony Mavunde, amezitaka kampuni na taasisi zilizokuwa zimefunga shughuli zake kwa sababu ya janga la virusi vya corona, kusaidia wafanyakazi wake baada ya huduma kurejea.

Mavunde alitoa rai hiyo jana wakati akizindua kurejeshwa kwa huduma za Hoteli ya Serena ya jijini Dar es Salaam, iliyokuwa imefungwa miezi michache iliyopita kutokana na janga la corona, tatizo ambalo pia limeziathiri hoteli na taasisi nyingine nchini na duniani kwa ujumla.

Alisema kuna kila sababu kwa kampuni hizo kuweka utaratibu utakaosaidia kurejesha hali za wafanyakazi wao ikiwamo kuwalipa mishahara baada ya mambo mengi kwenda kombo kipindi cha corona.

“Tunajua mambo mengi yalikwenda tofauti kipindi cha janga la corona, hatua iliyosababisha hata baadhi ya kampuni kushindwa kuwalipa mishahara wafanyakazi wake, lakini kwa kuwa sasa mambo yamerudi ni vyema zikawalipa ili waweze kujikwamua na hali ya kimaisha,” alisema.

Aidha, Mavunde alitoa rai kwa Watanzania kujenga utamaduni wa kutembelea vivutio mbalimbali vya utalii vilivyomo nchini ili kukuza utalii wa ndani badala ya kuwaachia wageni kutoka nje pekee.

Naibu Waziri huyo alipomngeza Rais John Magufuli, kwa jitihada mbalimbali za kukuza utalii na kuinua maisha ya Watanzania kupitia sekta hiyo.

Alisema katika kipindi cha miaka mitano ya utawala wa Rais Magufuli, Tanzania imepiga hatua kubwa katika sekta ya utalii na hivyo kuwavutia wageni wengi kutoka mataifa mbalimbali.

Meneja Mauzo na Masoko wa Serena, Seraphin Lusala, alisema kufunguliwa kwa hoteli hiyo kunatoa fursa nyingine ya kuendelea kuwahudumia wateja mbalimbali, wakiwemo wageni wanaokuja nchini kwa ajili ya kufanya utalii.

Alisema mbali hoteli hiyo tawi la Dar es Salaam kurejesha huduma, pia matawi yake mengine yaliyopo Ngorongoro, Manyara na katika Hifadhi ya Taifa ya Nyerere (Selous), yanaendelea kupokea watalii, huku akitangaza punguzo la bei hususani kwa watalii wa ndani kwa lengo la kuwahamasisha kwenda kuzitembelea.

Pia wadau mbalimbali walichanga hadi ujenzi ukafikia hatua ya kuezekwa ...

foto
Mwandishi: Oscar Job

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi