loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Jela miaka 12 kwa kuhujumu Tanesco

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam, imewahukumu mafundi umeme wawili na mmiliki wa nyumba kutumikia kifungo cha miaka 12 jela na mmiliki huyo kulipa faini ya Sh milioni mbili, baada ya kuwakuta na hatia ya kuingilia miundombinu ya umeme.

Washitakiwa hao ni Jiddah Abdallah na Abel Myonga ambao ni mafundi umeme na Hashim Rwambo ambaye ni mwenye nyumba aliyeunganishiwa umeme kinyume cha utaratibu.

Washitakiwa hao walihukumiwa jana bila wao kuwepo mahakamani.

Akisoma hukumu hiyo, Hakimu Mkazi Mkuu, Richard Kabate, alisema upande wa mashitaka ulipeleka mahakamani hapo mashahidi watatu kwa ajili ya kuthibitisha mashitaka hayo na kwamba baada ya ushahidi kutolewa, washitakiwa hawakuonekana tena mahakamani.

Alisema juhudi za kuwapata wadhamini zilishindikana, hivyo mahakama ilitoa hukumu pasipo kuwepo washitakiwa.

“Mahakama inawatia hatiani washitakiwa wote na kuwapa adhabu, mshitakiwa wa kwanza na wa pili kutumikia kifungo cha miaka 12 jela na mshitakiwa wa tatu anatakiwa kulipa fidia ya Sh milioni mbili na adhabu zao zitaanza pindi watakapopatikana,” alisema Hakimu Kabate.

Kabla ya kutolewa kwa hukumu hiyo, Wakili wa Serikali, Janeth Magoho, aliomba Mahakama kutoa adhabu kali kwa mshitakiwa ili iwe fundisho kwa wengine.

Katika hati ya mashiraka, ilidaiwa katika tarehe isiyofahamika Agosti, 2016, maeneo ya Mbezi Juu Goba kwa Sanya, wilayani Kinondoni, washitakiwa hao waliingilia miundombinu ya umeme kwa kumuunganishia umeme Rwambo.

OFISI ya Wakili Mkuu wa Serikali imesema haitasita kuwasilisha rufaa ...

foto
Mwandishi: Francisca Emmanuel

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi