loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Magari yote SMZ kuhakikiwa bima

MAKAMU wa Pili wa Rais, Balozi Seif Ali Iddi, amewaagiza makamanda wa polisi mikoa ya Zanzibar kuhakiki magari yote za serikali na taasisi zake kuona kama yamekatiwa bima kwa mujibu wa sheria na maelekezo ya serikali.

Balozi Iddi alitoa agizo hilo jana katika kilele cha Siku ya Bima kwenye Uwanja wa Gombani, Pemba.

Alisema uamuzi wa magari yote ya serikali na taasisi na mashirika ya umma kukatiwa bima umefikiwa na serikali na unatakiwa utekelezwe kwa mujibu wa sheria.

“Haipendezi hata kidogo kuona serikali imeweka sheria ya magari ya serikali kukatiwa bima halafu agizo hilo halitekelezwi.”

“Natoa agizo kuwataka makamanda wa polisi wa mikoa mitano ya Unguja na Pemba kukagua magari yote ya serikali, ambayo hayajakatiwa bima zichukuliwe hatua kwani serikalini tayari tumepitisha sheria ya magari hayo kukatiwa bima.”

“Kwa mfano, taasisi zote za serikali zimekuwa na utamaduni wa kuomba fedha katika bajeti za wizara kwa ajili ya vyombo vyao kukatiwa bima,” alisema.

Naibu Kamishna wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bima nchini, Khadija Issa Said, alisema kila chombo kinachotembea barabarani, baharini na angani kinatakiwa kukatiwa bima kwa mujibu wa sheria.

Alisema wamefanya uchunguzi na kubaini wapo watu wengi wanaoendesha vyombo vya moto barabarani huku vikiwa havijakatiwa bima na hivyo kusababisha usumbufu mkubwa wakati wa madai ya ajali.

“Sheria yetu inavitaka vyombo vyote vinavyotembea barabarani pamoja na baharini na angani kuhakikisha vinakata bima ili kurahisisha malipo wakati wa ajali,” alisema.

Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba, Hemed Suleiman, alisema kutokana na ukuaji wa wa huduma za kiuchumi na uwekezaji katika kisiwa cha Pemba, huduma za bima zinahitajika kwa kiwango kikubwa.

“Tunahitaji huduma zaidi za kampuni za bima katika kisiwa cha Pemba. Tayari yapo mashirika mawili na wakala watano wanaofanya kazi za bima,” alisema.

Wagombea kutoka vyama vya ...

foto
Mwandishi: Khatib Suleiman, Zanzibar

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi