loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Burundi yatangaza hatua kudhibiti corona

UONGOZI mpya wa Burundi umetangaza hatua nne ukudhibiti maambukizi mapya ya virusi vya corona na kuweka mkazo wa utekelezaji hatua hizo ikiwamo kupunguza asilimia 50 bei ya sabuni.

Akihutubia Bunge baada ya kuapishwa kwa mawaziri, Rais Evariste Ndayishimiye alitangaza hatua hizo na kusema mamlaka zitahakikisha watu wengi wanapata sabuni.

“Hii ni kuhakikisha asilimia kubwa ya watu wanaweza kupata sabuni, hivyo bei ya bidhaa hiyo imepungua kwa asilimia 50 na nusu ya gharama iliyobaki itabebwa na Serikali ili kuzuia viwanda visikwame katika uzalishaji.

“Mtu yeyote atakayepatikana akifanya biashara ya magendo kwa bidhaa hiyo ya sabuni kutoka Burundi, atachukuliwa kama msambazaji wa virusi vya corona na hatua kali dhidi yake zitachukuliwa,” alisema Rais Ndayishimiye.

Hatua ya pili ni kupunguza bei ya maji katika miji yote nchini mpaka corona itakapodhibitiwa, hatua ya tatu ni kuwataka wote watakaojisikia dalili za homa kali ya mapafu inayosababishwa na virusi hivyo (Covid-19) kwenda hospitali kupimwa na kutibiwa bila malipo wakiumwa.

Rais Ndayishimiye aliitaja hata ya nne kuwa ni kuwapima watu wote wakazi wa eneo alikotoka muathirika wa Covid-19 ili kupunguza kasi ya maambukizi ya ugonjwa kudhibiti eneo husika.

Wagombea kutoka vyama vya ...

foto
Mwandishi: BUJUMBURA, Burundi

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi