loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Kairuki ataka sheria, staha kutatua migogoro

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji), Angellah Kairuki amesisitiza kwa viongozi mbalimbali nchini kutochukua sheria mkononi kwa wawekezaji, bali wanapotaka kuamua mambo ni lazima wazingatia haki, staha na sheria kwa ajili ya kutatua migogoro.

Aidha, taasisi inayojishughulisha na Kilimo cha Mbogamboga, Maua, Matunda, Viungo na Mazao ya Mizizi (TAHA) ipo katika mchakato wa kufanya tafiti za kilimo katika maeneo ambayo yanalima mazao mbalimbali sambamba na changamoto za usafirishaji katika sekta ya anga, bandari pamoja na barabara.

Kairuki aliyasema hayo jana hapa wakati alipokagua mashamba ya maua, pamoja na Taha inayosimamia wakulima mbali mbali kwa ajili ya kuhakikisha sekta hiyo inakua na kuinua uchumi wa nchi.

Alisema serikali inathamini wawekezaji na ndio maana wamesogeza huduma za uwekezaji kwa kila mkoa kuhakikisha uwekezaji unakua kwani kasi kubwa, huku akisisitiza kuna taratibu za kuchukua kwa wawekezaji ambao hata kama wanakosea lakini ni vema taratibu zikafuatwa kwa staha.

Pia alitoa rai kwa Taha kuwekeza zaidi katika Kisiwa cha Mafia mkoani Pwani kwani kuna fursa mbali mbali za uwekezaji ikiwemo fursa za utalii pamoja na fursa za kilimo.

Pia alisisitiza kuhusu usafirishaji wa huduma za ndege, akisema serikali imenunua ndege hivyo suala la changamoto za usafirishaji wa bidhaa nje ya nchi zitatatuliwa ili kufunga fursa za kibiashara zilizopo ughhaibuni.

Alisisitiza mafunzo ni muhimu kuwezesha wanafunzi kujua aina za maua zinazopakana nchini na soko kwa ujumla, na kuwa Taha watakaoufanya uangalie zaidi fursa za kilimo kila mkoa kwa kushirikiana na wakulima, wizara mbali mbali kujua aina za mazao zitakazolimwa nchini.

Mkurugenzi wa Taha, Jackline Mkindi alisema wapo mbioni kufanya tafiti ili kujua changamoto wanazokumbana nazo katika sekta ya usafirishaji ikiwemo katika bandari na anga.

MAKAMU wa Pili wa Rais, Balozi Seif Ali Iddi amesema ...

foto
Mwandishi: Veronica Mheta, Arusha

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi