loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Tanelec waagizwa kujitangaza EAC

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji), Angellah Kairuki ameitaka Kampuni ya Tanelec inayozalisha transfoma katika nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), kujitangaza zaidi na kupata masoko ili kuongeza tija katika ukuaji wa uchumi.

Kairuki aliyasema hayo jana wakati alipozuru kiwanda hicho kilichopo Themi jijini hapa kujionea shughuli mbali za uzalishaji wa transfoma pamoja na changamoto wanazokumbana nazo katika uzalishaji.

Alisema kampuni hiyo ambayo ni mbia na serikali inajitahidi kuhakikisha inatengeneza transfoma nyingi kuwezesha Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) kusambaza umeme.

Alisema hadi kufikia Juni 29, mwaka huu serikali imefanikisha kusambaza umeme kwa vijiji 9,314 ikilinganishwa na vijiji 2,018 vilivyokuwa vimeunganishwa umeme mwaka 2018 sawa na ongezeko la asilimia 361.5 kupitia Mpango Kabambe wa Usambazaji Umeme Vijijini.

Alisema tangu Rais Magufuli alipoingia madarakani hadi sasa, wateja zaidi ya milioni 2.7 wamepata umeme huku akiwasisitiza kuendelea kufanya tafiti za kimasoko ili kuona uhitaji wa transfoma katika EAC na nchi nyingine.

“Nawapongeza kwa kuzalisha transfoma hizi lakini endeleeni kuendelea kutengeneza transfoma na kupata masoko zaidi katika nchi za EAC, pia fanyeni tafiti zaidi za masoko ili kuuza zaidi transfoma hizi zinazozalishwa Tanzania,” alieleza Kairuki.

Mkurugenzi Mkuu wa Tanelec, Zahir Saleh alisema wanalazimika kununua waya aina ya enamael kutoka nje ya nchi kwa gharama kubwa ingawa Tanzania kuna viwanda vinne vinavyotengeneza waya ila hawatengenezi waya aina hiyo ndio maana wanaagiza nje ya nchi.

SIKU zinahesabika ndani ...

foto
Mwandishi: Veronica Mheta, Arusha

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi