loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Wafanyakazi TBS hatarini kufukuzwa kazi

WAZIRI wa Viwanda na Biashara, Innocent Bashungwa amemuagiza Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS) kuwafukuza kazi wafanyakazi wa shirika hilo wanaowatoza fedha na wanaochelewesha kutoa nembo ya ubora kwa bidhaa zinazotengenezwa kwenye viwanda vidogo nchini.

Bashungwa ametoa maelekezo hayo juzi alipofanya ziara mkoani Simiyu na kutembelea kiwanda cha usindikaji wa viazi lishe kilichopo Wilaya ya Maswa kinachojulikana kwa jina la Ng’hami Industries Company Ltd.

Amefikia uamuzi huo baada ya kufika kiwandani hapo na kukagua bidhaa za kiwanda hicho ambayo ni unga wa viazi lishe na kugundua hazina nembo ya ubora ya TBS, kutokana na wafanyakazi wa TBS kuwaomba fedha kwa ajiri ya kupewa nembo ya ubora pia kuchelewesha kwa zaidi ya miezi saba bila kupewa majibu au nembo ya ubora.

Baada ya kuona changamoto hiyo, Bashungwa alimpigia simu Mkurugenzi Mkuu wa TBS, Dk Yusuph Ngenya na kumuelekeza kuwafukuza kazi wafanyakazi wake wanaokwenda kinyume cha maagizo ambayo amekuwa akiyatoa mara kwa mara ya kutowachelewesha wafanyabiashara kwa sababu zisizo za msingi.

Amesema sababu hizo zinasababisha bidhaa kutopewa nembo za ubora kwa wakati ambazo zinasababisha mazingira ya rushwa na usumbufu kwa wazalishaji wa bidhaa mbali mbali.

Mkurugenzi Mtendaji wa kiwanda hicho, Ntobi Rufunga alisema barua ya kuomba nembo ya ubora ilipelekwa TBS tangu Novemba mwaka jana, lakini hadi sasa hajapewa majibu yoyote na baada ya kuchukuliwa kwa sampuli ya bidhaa hiyo wameombwa kutoa Sh 520,000 ili wapewe nembo ya ubora, kinyume cha sheria na masharti ya TBS.

Aidha, Ntobi alisema kiwanda hicho mpaka sasa kinazalisha unga wa viazi lishe wa aina mbili ambao ni unga wa kupika uji kwa ajili ya matumizi ya rika zote, na unga wa kutengeneza keki, mikate na andazi.

KATIBU Tawala Mkoa wa Kagera, Profesa Faustine Kamuzora, amewaomba wamiliki ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Maalumu, Maswa

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi