loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Wanafunzi 40 wajazwa mimba Bunda

SERIKALI wilayani Bunda mkoani Mara imeanzisha msako kuwatafuta wanaotuhumiwa kuwapa ujauzito wanafunzi zaidi ya 40.

Hali hiyo imegundulika wakati wanafunzi wakianza kuripoti shuleni kuanzia wiki hii kwa shule za msingi na sekondari wilayani hapa baada ya likizo ya lazima ya corona.

Mkuu wa Wilaya ya Bunda, Lydia Bupilipili alisema wakati akipokea ripoti ya utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM kwa Serikali ya Awamu ya Tano. Alisema kuna maeneo kuna wasiwasi huenda idadi hiyo ikaongezeka.

Alieleza kuwa kuanzia Januari hadi Juni mwaka huu, wanafunzi wa shule za msingi na sekondari 26 walipata ujauzito huku visa vingine 19 vya ubakaji vikiripotiwa wilayani hapa.

“Serikali imeanzisha msako mkali kwa wale wote waliohusika na unyanyasaji huu kwa namna moja au nyingine wakiwemo wazazi wanaodaiwa kuwaozesha mabinti hao na kupokea mahari,” alisema Bupilipili.

Alisema katika kipindi cha miaka mitano iliyopita, miradi yenye thamani ya Sh bilioni 80 imetekelezwa wilayani hapa ikiwemo ya elimu, afya, barabara na maji.

Kulingana na asasi za kiraia zinazotetea haki za wanawake na watoto wilayani humo, sababu zinazohusishwa na kuongeza visa vya ukatili huo dhidi ya watoto ni pamoja na imani za kishirikina na umasikini.

Mkurugenzi wa shirika lisilo la kiserikali la Kivulini, Yassin Ally alisema asasi hiyo imefadhili masomo ya mtoto mmoja aliyedaiwa kubakwa na baba yake mzazi hadi ngazi ya chuo kikuu.

SIKU zinahesabika ndani ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu, Bunda

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi