loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Aga Khan kutumia mil 780/- kuanzisha kitengo

HUDUMA za Afya Aga Khan Tanzania na Shirika la Maendeleo la Ufaransa (AFD) wamesaini makubaliano ya kutumia Sh milioni 780 kuanzisha kitengo cha Magonjwa yasiyoambukiza (IDU) jijini Dar es Salaam na Mwanza.

Kitengo hicho kitatoa huduma , kitajenga uwezo, miundombinu na teknolojia ili kuboresha ubora wa utoaji huduma kwa ufadhili wa ruzuku ya Euro 300,000 kutoka Shirika la AFD.

Makubalino ya kuanzisha kitongo hicho yamesainiwa na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Huduma za Afya Aga Khan Kanda ya Afrika Mashariki, Sulaiman Shahabuddin na Mkurugenzi Mkazi wa AFD nchini Tanzania, Stéphanie Mouen.

Imeelezwa kuwa mpango huo umeanzishwa na Huduma za Afya Aga Khan (AKHS), AFD na wabia wengine na kutumia ruzuku hiyo kwa kuimarisha mfumo wa sasa ili kushughulikia changamoto zinazohusiana na usimamizi wa udhibiti wa magonjwa yanayoambukiza.

“Itaiwezesha Hospitali ya Aga Khan, Dar es Salaam kuitikia vya kutosha suala la magonjwa-tandavu, kama vile Covid 19 , ikiwemo kushughulikia masuala yanayohusiana na uhaba wa miundombinu na uwezo wa huduma za afya,” amesema Shahabuddin.

Amesema fedha zilizotolewa na AFD ni kama sehemu ya mpango wa kimataifa unaojulikana kama “COVID 19– Health in Common” ulioanzishwa na Rais wa Ufaransa na kutekelezwa na AFD kama mwitikio wa janga la kiulimwengu la afya ya umma linalosababishwa na magonjwa-tandavu yanayoenea duniani kote.

Mpango huo pamoja na mambo mengine una lengo la kuendeleza miundombinu, kuboresha huduma na majengo , kujenga uwezo na teknolojia kwa kutumia teknolojia na kuimarisha uunganishaji wa huduma ya afya kwa njia ya mtandao kati ya hospitali nyingine na IDU.

Shahabuddin amesema AKHST inawahudumia Watanzania kwa zaidi ya miaka 90, ikishirikiana na Serikali kupitia uhusiano wa ubia wa Serikali na sekta binafsi (PPP).

Taasisi hiyo inatumika kama kituo cha matibabu kinachounga mkono uwekaji mipango wakati wa dharura na ufikiaji wa huduma zenye mantiki na zinazozingatia muda kwa wagonjwa.

Amesema kitengo cha IDU kitawezesha ushirikiano zaidi na jitihada za pamoja katika kudhibiti, kuzuia maambukizi, kuwatenga na matibabu kwa wagonjwa, na mwitikio wa mfumo wa afya.

“Kitengo hiki kipya kwenye Hospitali ya Aga Khan ambayo ni hospitali ya rufaa ya kanda kitatumia uwezo wake wa kiufundi na utekelezaji kupitia mipango iliyopo sasa ya utoaji wa tiba na huduma za usaidizi ili kutekeleza afua zilizopangwa za matibabu kwa wagonjwa wa maradhi yanayoambukiza,” alisema.

Mwakilishi wa AFD Tanzania kwenye hafla hiyo Mouen amesema shirika hilo linaamini kuwa mpango huo utadhihirisha mwitikio na ufanisi katika kuunga mkono maendeleo ya wabia hao hasa katika Kanda ya Afrika Mashariki.

Amesema, ubia huo ni wa uhakika ili kuleta matokeo yanayotarajiwa na ulianza zaidi ya miaka 12 iliyopita ambapo AFD Group na AKDN walisaini makubaliano ya ushirikiano ili kuwa na maslahi ya pamoja na shauku ya dhati ya kuwekeza katika ukuaji wa kijamii na kuboresha maisha ya watu.

Sambamba na mipango inayoendeshwa na Ufaransa katika ngazi mbalimbali, mradi huo unadhihirisha azimio la kuisaidia Tanzania hasa katika kukabili janga la ugonjwa wa Covid 19 unaosababishwa na virusi vya corona.

SIKU zinahesabika ndani ...

foto
Mwandishi: Theopista Nsanzugwanko

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi