loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Waziri: Tumeeni viwanda kukuza uchumi binafsi

WAZIRI wa Viwanda na Biashara, Innocent Bashungwa amesema mikakati endelevu kwenye sekta ya viwanda itatakayokuwa ikitekelezwa na Serikali itazidi kuimarisha uchumi wa kila mwananchi .

Akizungumza jana kwenye Maonesho ya 44 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (DITF), Waziri Bashungwa alieleza kuwa kufikia kwenye uchumi wa kati umechangiwa na mengi na kwamba wananchi wana nafasi kubwa zaidi ya kukuza vipato vyao iwapo tutaendelea kuwekeza kwenye viwanda na uzalishaji mali.

"Uchumi wa kati tumeufikia kabla ya muda utuliokuwa tumepanga (kabla ya 2025), hivyo sasa tujikite kuendeleza sekta ya viwanda ili uchumi na kipato cha wananchi kiendelee kuwa bora, " alisema Waziri Bashingwa.

 Aidha, Waziri huyo alianisha kuwa miongoni mwa mambo yaliyoibeba nchi kuelekea uchumi wa kati ni miundombinu na mazingira wezeshi kwa wenye viwanda.

“Miundombinu bora kama barabara, reli na uwepo wa huduma za ndege za uhakika zimekuwa na chachu kuipeleka Tanzania kwenye uchumi wa kati,"alisema Bashungwa.

Waziri huyo pia ametangaza nia ya kuendelea kuliwakilisha  Jimbo la Karagwe na kwamba kama wananchi wake watapendezwa badi atagombea kwenye uchaguzi mkuu Oktoba mwaka huu.

KATIBU Tawala Mkoa wa Kagera, Profesa Faustine Kamuzora, amewaomba wamiliki ...

foto
Mwandishi: Alfred Lasteck

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi