loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Wateja wa 'Luku' kupigwa simu uniti zinapokaribia kuisha

HUENDA ikaonekana ni kama miujiza lakini teknolojia na umahiri wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) kwenye masuala ya ubunifu kwenye sayansi sasa inamwezesha mteja wa huduma za umeme kujua kuwa nishati hiyo inakaribia kuisha.

Chui hicho kimebuni  kifaa kinachompigia simu mteja wa umeme kumwambia kiwango cha umeme kilichobaki hivyo kumsaidia kuondokana na adha ya kukaa gizani.

Akizungumzia ubunifu huo kenye viwanja vya Maonesho ya 44 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (DITF) yanayoendelea katika Viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam, Ofisa wa kutoka Idara ya Teknolojia chuoni hapo, Edson Nasolwa alisema ubunifu huo ulianza 2019 na umekamilika mwaka huu 2020.

Ofisa huyo alisema kifaa hicho ni muhimu na wameshafanya mazungumzo na Tanesco ili wakikubaliana kifaa hicho kiingizwe ndani ya mashine za Luku na kusambazwa kwa wateja wao.

 “Kifaa hiki kinaweza kuwasaidia wateja wa umeme kwa kuwapigia simu na kuwapa taarifa ya kiwango cha umeme ‘uniti’ kilichobaki kwenye Luku yake ili afahamu na kuchukua hatua ya kununua umeme kabla haujaisha,” alisema Nasolwa na kuongeza kuwa mfumo huo utapunguza usumbufu kwa watumiaji.

OFISI ya Wakili Mkuu wa Serikali imesema haitasita kuwasilisha rufaa ...

foto
Mwandishi: Alfred Lasteck

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi