loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Maharusi sasa ruksa kukodi farasi wa polisi

JESHI la Polisi nchini kupitia Kikosi cha Farasi kimeanzisha huduma ya kukodisha farasi kwa ajili ya shughuli mbali mbali za kijamii ikiwemo sherehe ya harusi.

Hayo yamebainishwa mapema leo na Mrakibu Msaidizi wa Polisi, ASP, Dk Omary Lunyombe akiwa kwenye  Viwanja vya Maonesho ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam maarufu Sabasaba.

Alisema farasi hao wamebobea katika utoaji wa huduma mbalimbali katika jamii kuanzia zinazohusiana na shughuli za kipolisi pamoja na masuala ya kijamii ikiwepo ubebaji wa raia.

“Kupitia uwezo wao, raia wanaweza kukodisha huduma za farasi. Kwa wapendanao hii ni huduma ya farasi wanaweza kuipata kwenye sherehe zao za kufunga ndoa,” alisema Lunyombe.

OFISI ya Wakili Mkuu wa Serikali imesema haitasita kuwasilisha rufaa ...

foto
Mwandishi: Alfred Lasteck

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi