loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

…Wachumi waeleza neema zitakazofuata

WATAALAMU wa uchumi wameendelea kuchambua hatua ya Tanzania kuondolewa kwenye kundi la nchi maskini, wakianisha neema zitakazofuata, baada ya Benki ya Dunia kuitangaza kuingia kundi la nchi za uchumi wa kati.

Wachambuzi wengi wamesema uongozi bora ni miongoni mwa vichocheo, vilivyoifikisha nchi katika kundi hilo, ambalo sasa wawekezaji kutoka sehemu mbali mbali duniani wataelekeza macho yao, wakiamini nchi ina soko na watu wenye uwezo wa kununua bidhaa.

“Watanzania wana kila sababu ya kutembea vifua mbele kwa sababu namba imetokana na nguvu zetu kama raia kama nchi. Ni jambo jema la kujivunia. Tukishaonekana tuko kwenye uchumi wa kati, ina maana tuna fedha za kuweza kutumia,” alisema mchambuzi wa masuala ya diplomasia na uchumi, Gabriel Mwang’onda.

Mwang’onda alisema hakuna mwekezaji anayetaka kufanya biashara na nchi masikini.

“Ukishatangazwa hivi, manufaa yake ni makubwa. Wawekezaji kutoka duniani kote wataweka jicho la ziada la uwekezaji, wakiamini kuna soko na watu na wenye uwezo wa kunununua,”alisema.

Alisema hatua ya serikali hususani Rais John Magufuli kuwa na msimamo wa maeneo ya utekelezaji kupitia bajeti mwaka hadi mwaka, imeinyanyua nchi kufikia hatua hiyo, ambayo ni ushindi mkubwa kwake, taifa na wananchi. Alitoa mfano wa wizara ambazo bajeti yake haijawahi kupungua tangu mwaka 2016 kuwa ni zinazohusika na miundombinu, nishati na elimu. Alisema kipindi kilichopita, kulikuwa na mabadiliko ya kiasi cha fedha kilichokuwa kikitengwa.

“Lakini katika awamu hii rais anasimamia mwenyewe vipaumbele anavijua na vimekuwa haviyumbi, vinasimamiwa inakuwa rahisi nchi kutoka sehemu moja kwenda nyingine,” alisema.

Alitoa mfano wa mpango wa utoaji elimu bila malipo, akisema serikali haijayumba katika utoaji fedha za kuufanikisha. Mhadhiri wa Chuo cha Diplomasia, Abbas Mwalimu alifafanua kwamba wastani wa pato la kila mwananchi, hupatikana kutoka katika pato la nchi kwa ujumla.

Hujumuisha mapato yote ya nchi yaliyozalishwa na wakazi wa nchi husika na biashara halali zilizomo ndani ya nchi na pato lililochumwa na raia wa nchi husika waliopo nje ya nchi.

Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma (Udom), Profesa Faustine Bee alitaja kitendo cha Tanzania kuingia rasmi katika kundi la nchi za uchumi wa kati ni hatua nzuri na kubwa, ambayo juhudi zikiwekwa zaidi, itakwenda katika kundi la nchi ya uchumi wa juu.

Pia wadau mbalimbali walichanga hadi ujenzi ukafikia hatua ya kuezekwa ...

foto
Mwandishi: Stella Nyemenohi

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi