loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Waziri Mkuu kufungua Maonesho ya Sabasaba leo

WARIZI Mkuu, Kassim Majaliwa, leo anafungua Maonesho ya 44 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (DITF) maarufu Sabasaba, yaliyoanza Julai Mosi na yatafungwa Julai 13, mwaka huu.

Akizungumza katika viwanja vya maonesho hayo jana,Waziri wa Viwanda na Biashara, Innocent Bashungwa, alitoa wito kwa wananchi kujitokeza kwa wingi kutembelea maonesho hayo ili kushuhudia ubunifu na teknolojia mpya zilizofanywa na Watanzania na washiriki wa nje.

Alisema maonesho hayo pia ni fursa nzuri kwa Watanzania kuyatumia kujifunza mambo mbalimbali ili kuongeza juhudi kwenye uzalishaji wa bidhaa hasa kwa kuwa nchi imeingia kwenye uchumi wa kipato cha kati.

“Nitumie fursa hii kumpongeza Rais John Magufuli kwa juhudi anazofanya nchini, ambazo zimewezesha sisi kuingia kwenye nchi ya uchumi wa kati, ukiangalia hayo yote ni kutokana na mambo mengi ikiwamo uboreshaji wa miundombinu nchini,” alisema.

Bashungwa alisema uwekezaji mkubwa unaofanywa nchini ikiwamo ujenzi wa reli ya kisasa, barabara na ununuzi wa ndege, umechangia nchi kupata kigezo cha kuingia hatua hiyo muhimu na sasa nguvu itaelekezwa zaidi kwenye sekta ya uzalishaji ambayo itasaidia kuinua maisha ya wananchi moja kwa moja.

“Uchumi wa viwanda tunaojenga lazima ubadilishe maisha na uchumi wa watu wetu yawe bora zaidi, uwapo wa miundombinu wezeshi uwe chachu ya wazalishaji kupitisha bidhaa zao kuyafikia masoko kiurahisi”, alisema Bashungwa.

Alisema Tanzania imeingia kwenye nchi za uchumi wa kipato cha kati miaka mitano kabla ya lengo, ambapo awali kwenye mpango wa taifa wa maendeleo, ilikuwa ifikapo mwaka 2025 nchi ndio ifike kwenye hatua hiyo.

“Utaona kwamba, lengo letu lilikuwa tuingie kwenye uchumi wa kati mwaka 2025, lakini tumefanikiwa kabla ya miaka mitano kufika, sasa miaka mitano iliyobaki tutaitumia kujenga uchumi endelevu baada ya kuwa na miundombinu wezeshi,” alisema.

Akizungumzia mipango ya baadaye ya wizara hiyo na kuboresha maonesho hayo, waziri huyo alisema wameshazungumza na wizara husika kuwa kila ofisi ya balozi wa Tanzania nje iwe na mwanadiplomasia wa biashara, ambaye atakuwa na kazi ya kutafuta masoko ya bidhaa za Tanzania kwenye nchi husika.

“Tumeshafanya utafiti na inawesekana kuwa na mwanadiplomasia wa biashara katika kila ubalozi wetu nje ili kazi yao iwe kutafuta masoko ya bidhaa za Tanzania, jambo hilo likitekelezwa lina manufaa kwa taifa,” alisema.

Aidha, Bashungwa aliitaka Mamlama ya Biashara Tanzania (TanTrade), ambayo ndio muandaaji wa maonesho hayo, kuwasisitiza washiriki na wajasiriamali nchini kutumia vifungashio vyenye ubora ili kuvutia bidhaa zao na kuziongezea thamani ziweze kupata masoko.

Pia wadau mbalimbali walichanga hadi ujenzi ukafikia hatua ya kuezekwa ...

foto
Mwandishi: Ikunda Erick

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi