loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Watanzania chapeni kazi - Magufuli

RAIS John Magufuli ametuma salamu kwa Watanzania, akiwataka wamuunge mkono na wachape kazi. Rais alitoa salamu hizo jana kupitia Msemaji Mkuu wa Serikali, Dk Hassan Abbasi, baada ya kumpigia simu yake ya mkononi wakati mkutano wa waandishi wa habari ukiendelea.

Akiwa katikati ya kuzungumzia Tanzania kuingia uchumi wa kati, Dk Abbasi alipokea simu na kusema: “Mheshimiwa Rais, naam, shikamoo, sijambo, niko kwenye press karibu sana kama una neno la kuwaambia Watanzania...

“Baada ya dakika kadhaa za kuzungumza na simu iliyopigiwa na Rais Magufuli, Dk Abbasi alisema: “Mheshimiwa Rais (John Magufuli) anawapa salamu, amefurahi sana na jana ali-twitt, amewataka Watanzania waendelee kumuunga mkono na kuchapa kazi.”

Juzi saa chache baada ya Benki ya Dunia kuitangaza Tanzania kuwa nchi ya uchumi wa kati kutoka nchi masikini duniani, Rais Magufuli kupitia ukurasa wake wa twitter aliwapongeza Watanzania wote.

Rais Magufuli alisema hatua hiyo ni matokeo ya jitihada na kufaya kazi kwa bidii kwa Watanzania wote. Rais alisema “Benki ya Dunia leo Julai 1, 2020 (juzi) imeitangaza Tanzania kuingia UCHUMI WA KATI. Nawapongeza Watanzania wenzangu kwa mafanikio haya. Huu ni ushindi mkubwa na kazi kubwa tumeifanya, tulipanga kuingia uchumi wa kati ifikapo 2025 lakini tumefanikiwa 2020. MUNGU IBARIKI TANZANIA.”

Pia wadau mbalimbali walichanga hadi ujenzi ukafikia hatua ya kuezekwa ...

foto
Mwandishi: Anastazia Anyimike, Dodoma

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi