loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Mabadiliko makubwa Dira ya Taifa ya mwaka 2025

DIRA ya Maendeleo ya Taifa 2025 inasisitiza kuwa ifi kapo 2025, Tanzania itakuwa imepitia mabadiliko makubwa ya kiuchumi na maendeleo ili kupata hali ya kipato cha kati, ikiwa na viwango vya juu vya viwanda, ushindani, maisha bora, utawala wa sheria na kuwa na jamii iliyoelimika na inayopenda kusoma.

Dira hiyo pia imeeleza kuhusu matarajio ya kijamii, kiuchumi na kisiasa nchini katika robo ya kwanza ya Karne ya 21 kwa lengo la kufikia hali ya kipato cha kati nchini, kwa kuwa na pato la kila mtu la Dola za Marekani 3,000 ifikapo mwaka 2025.

Hivi sasa Tanzania imeshaingia uchumi wa kati, baada ya kutangazwa juzi na Benki ya Dunia na kisha Rais John Magufuli kulitangazia taifa kwa mafanikio hayo.

Kama Dira ya Maendeleo ilivyobainisha kuwa ili kufikia uchumi wa kati, taifa linahitaji kufanya mabadiliko makubwa ya kiuchumi na maendeleo, miongoni mwa mabadiliko hayo ambayo Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais Magufuli imeyatekeleza ni ujenzi wa miundombinu mikubwa na ya kisasa ya reli (SGR), umeme na kuimarisha sekta ya anga.

Ujenzi wa SGR yenye urefu wa kilometa 300 kutoka Dar es Salaam mpaka Morogoro, umefikia asilimia 82 mpaka sasa. Kutoka Morogoro hadi Makutupora mkoani Dodoma, urefu wa kilometa 422, ujenzi huo umefikia asilimia 34. Kwa pamoja ujenzi huo unagharimu zaidi ya Sh trilioni 7, ambazo ni fedha za serikali.

Akiwa wilayani Kilosa mkoani Morogoro mwanzoni mwa wiki hii, Rais John Magufuli alisema ujenzi wa reli hiyo kwenda Mwanza, utaanza mwaka huu wa fedha. Baadaye itajengwa kwenda Kigoma na Katavi.

Reli hiyo ambayo inajengwa na Kampuni ya Yapi Merkezi ya Uturuki, itakuwa na uwezo wa kupitisha treni zenye uwezo wa mwendokasi wa Kilomita 160 kwa saa, kupitisha mzigo wa tani kati ya milioni 17 hadi 25 kwa mwaka.

Mradi mwingine mkubwa ni uzalishaji wa umeme wa maji wa Julius Nyerere katika Mto Rufiji mkoani Pwani. Mradi huo utakuwa na uwezo wa kuzalisha Megawati 2,115 za umeme na unajengwa na Kampuni ya J.V Arab Contractors/El Sewedy Electric ya Misri kwa gharama ya Sh trilioni 6.6, ambazo ni fedha za serikali.

Serikali pia inatekeleza mradi wa umeme vijijini (REA), ambapo mpaka sasa vijiji 9,000, kati ya 12,000, vimeshaunganishwa na nishati hiyo. Vijiji 3,000 vilivyobaki vitaunganishwa na nishati hiyo mwaka huu wa fedha.

Katika usafiri wa anga, serikali imefanikiwa kuifufua Kampuni ya Ndege (ATCL) kwa kununua ndege mpya nane zikiwemo Boeing 787-8 Dreamliner mbili, Airbus A220-300 mbili na Bombardier Dash 8 Q400 nne.

Pia wadau mbalimbali walichanga hadi ujenzi ukafikia hatua ya kuezekwa ...

foto
Mwandishi: Matern Kayera

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi