loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Majimbo 4 ya uchaguzi Z’bar yafutwa

TUME ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) imefanya mapitio ya idadi, majina na mipaka ya majimbo ya uchaguzi Zanzibar kwa mujibu wa Kifungu cha 120 (4) cha Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 na kuyafuta majimbo manne.

Hivyo majimbo ya uchaguzi ambayo yatakayotumika katika Uchaguzi Mkuu mwaka huu ni 50 badala ya 54 yaliotumika katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015.

Mwenyekiti wa ZEC, Jaji mstaafu Hamid Mahmoud alisema mwaka 2015 majimbo yalikuwa 54, ambayo mabadiliko yalilalamikiwa na wadau wa uchaguzi na kusababisha usumbufu kwa wapiga kura kwa baadhi ya majimbo.

Aliyataja majimbo yaliyofutwa ni Jimbo la Kiwengwa, Mtopepo, Kijitoupele na Chukwani, na hivyo sasa Wilaya ya Magharibi B kutakuwa na majimbo matano badala ya saba na Kaskazini B kutakuwa na majimbo matatu badala ya manne na Magharibi A kutakuwa na majimbo matano badala ya sita.

Majimbo yaliyofutwa yalikuwa yakishikiliwa na Wawakilishi kutoka Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambako kwa upande wa Kisiwa cha Pemba, Jimbo la Mgogoni limefutwa na kubadilishwa jina la Jimbo la Pandani.

Alisema wadau wa uchaguzi waliibua changamoto ya uwepo wa tofauti kubwa ya wapiga kura kati ya jimbo moja na jimbo jingine na ndiyo maana wamekuja na mabadiliko ya kufuta baadhi ya majimbo ya uchaguzi.

Alisema kuelekea Uchaguzi Mkuu mwaka huu ZEC ilizijadili kwa kina changamoto hizo na iliamua kwa mamlaka iliyonayo kufanya uchunguzi wa kina juu ya madai ya changamoto zilizotolewa na wadau kwa lengo la kujiridhisha kama kweli kuna changamoto.

“Katika kazi hiyo, tume iliangalia kigezo cha idadi ya watu katika majimbo na uwakilishi unaofaa katika miji mikubwa na miji ya mashamba yenye idadi ndogo ya watu...kwa hivyo Tume ya Uchaguzi imefuta majimbo manne yaliopo Unguja wakati Pemba yatabakia majimbo 18 kama ilivyokuwa zamani,” alisema Jaji Mahmoud.

Alifafanua kuwa uchunguzi huo unaonesha idadi ya watu wanaohamia katika miji ya mashamba kutokana na sababu mbali mbali za kiuchumi na kijamii inaongezeka kwa kasi sana katika maeneo ya Wilaya ya Magharib A na B Unguja, Wilaya za Wete na Mkoani, Chake Chake Pemba.

“Katika Kisiwa cha Pemba yatabakia majimbo 18 kama ilivyokuwa katika uchaguzi wa mwaka 2015 lakini tumelifuta Jimbo la Mgogoni na kulipa jina la Pandani lililopo Mkoa wa Kaskazini Pemba,” alisema Jaji Mahmoud.

Pia wadau mbalimbali walichanga hadi ujenzi ukafikia hatua ya kuezekwa ...

foto
Mwandishi: Khatib Suleiman, Zanzibar

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi