loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Magufuli aipongeza sekta ya fedha Tanzania kufikia uchumi wa kati

Rais John Magufuli ameipongeza Benki Kuu (BOT), sekta ya benki na fedha kwa ujumla kutokana na mchango wao katika kuiwezesha Tanzania kuingia katika kundi la nchi za uchumi wa kati.

Dk Magufuli ametoa pongezi hizo katika mazungumzo yake na Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Prof. Florens Luoga. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Idara ya Uhusiano na Itifaki ya BOT, Rais Magufuli amemtaka Gavana Luoga kumfikishia salamu zake za pongezi kwa wafanyakazi wa Benki Kuu na kwa sekta ya fedha kwa ujumla.

Aidha, amezitaka Benki Kuu, benki nyingine pamoja na sekta ya fedha kuendelea kuchapa kazi kwa bidii na weledi kwa maendeleo ya nchi. Mnamo Julai 1, 2020, Benki ya Dunia ilitangaza kwamba Tanzania imeingia katika kundi la nchi za uchumi wa kati.

“Benki ya Dunia inaitambua nchi kwamba imeingia katika kundi la chini la nchi za uchumi wa kati kama wastani wa pato la mtu kwa mwaka ni kati ya dola za Kimarekani 1,036 na dola 4,045,” taarifa hiyo imeeleza.

MGOMBEA urais wa ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi

Magufuli: Nataka kumalizia kazi

masaa 2 yaliyopita Magnus Mahenge, Dodoma

MGOMBEA urais wa ...

Wanawake waihakikishia CCM ushindi

masaa 2 yaliyopita Magnus Mahenge, Dodoma

 

Waziri aagiza mifumo ya fedha ipunguze rushwa

masaa 4 yaliyopita Mwandishi Maalumu, Simiyu

WAZIRI ...