loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Mchujo wanaowania Urais Zanzibar leo

KAMATI Maalumu ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi, Zanzibar, inatarajiwa kuanza kikao chake leo, kupitia majina ya wanachama wa chama hicho 31, walioomba ridhaa ya kuwania nafasi ya urais wa Zanzibar.

Kikao hicho kinafanyika baada ya kufanyika kwa kikao cha Kamati ya Maadili na Usalama kwa muda wa siku mbili. Miongoni mwa majukumumu ya kikao hicho ni kupitia majina ya wanachama wote, walioomba ridhaa ya kuwania nafasi ya urais na kuangalia sifa zao na kuona kama wanakidhi vigezo, vilivyowekwa vya ongozi wa umma na ndani ya Chama. Imeelezwa kuwa kikao hicho kilipitia fomu za maombi ya wanachama, kuona kama taratibu zote zilizoagizwa kwa waliochukua fomu zimezingatiwa.

Taratibu hizo ni kuona kama wamepata wanachama wadhamini kutoka katika mikoa mitatu ya Zanzibar, ikiwemo mmoja kutoka Pemba. Katibu wa Idara ya Itikadi na Uenezi ya chama hicho, Zanzibar, Caterina Peter, akizungumza na gazeti hili, alisema kwamba baada ya kikao cha Kamati ya Maadili, sasa kinafanyika kikao cha Kamati Maalumu, ambacho kitaongozwa na Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, Rais Dk Ali Mohamed Shein.

“Kikao hicho kwa ufupi kilikuwa na kazi ya kuyapitia majina yote ya wanachama wa CCM, wenye nia ya kupeperusha bendera ya chama katika kinyang’anyiro cha urais wa Zanzibar kuangalia sifa na vigezo vinavyotakiwa kabla ya kuyapeleka kwa Kamati Maalumu ya Halmashauri Kuu ya CCM Zanzibar”alisema.

Wanachama 31 watakaojadiliwa ambao walichukua fomu ni: Mbwana Bakari Juma, Ali Abeid Karume, Mbwana Yahya Mwinyi, Omar Sheha Mussa, Hussein Ali Mussa na Shamsi Vuai Nahodha.

Wengine ni Mohamed Jafaar Jumanne, Mohamed Haji Mohamed, Issa Suleiman Nassor, Makame Mnyaa Mbarawa, Mwatum Mussa Sultani, Haji Rashid Pandu, Abdulhamid Mohamed Ali, Jecha Salum Jecha na Dk Khalid Salum Mohamed.

Wanachama wengine Rashid Ali Juma, Khamis Mussa Omar, Mmanga Mjengo Majwiri, Hamad Yussuf Masauni, Mohamed Aboud, Bakari Rashid Bakari, Ayoub Mohamed Mahmoud, Hashim Salum Hashim, Hasna Attai Masoud, Fatma Kombo Masoud, Pereira Ame Silima, Iddi Hamad Iddi, Shaame Simai Mcha, Mussa Aboud Jumbe, Mgeni Hassan Juma na Maudline Castico.

Alisema kuwa maandalizi yamekamilika na kwmaba wajumbe kutoka kisiwa cha Pemba, tayari wapo Zanzibar kwa ajili ya mkutano huo. Kikao hicho cha Kamati Maalumu ya Halmashauri Kuu ya CCM kinatarajiwa kuhudhuriwa na Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan ambaye yupo Zanzibar akikamilisha ziara ya kichama ya mikoa minne.

MGOMBEA urais wa ...

foto
Mwandishi: Khatib Suleiman, Zanzibar

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi

Magufuli: Nataka kumalizia kazi

masaa 2 yaliyopita Magnus Mahenge, Dodoma

MGOMBEA urais wa ...

Wanawake waihakikishia CCM ushindi

masaa 2 yaliyopita Magnus Mahenge, Dodoma

 

Waziri aagiza mifumo ya fedha ipunguze rushwa

masaa 5 yaliyopita Mwandishi Maalumu, Simiyu

WAZIRI ...