loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Andengenye awa RC mpya Kigoma, Mwanri astaafu

RAIS John Magufuli amefanya uteuzi wa wakuu wa mikoa wawili na wakuu wa wilaya tisa. Miongoni mwa watu hao ni aliyewahi kuwa Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji,Thobias Andengeye (pichani) aliyeteuliwa kuwa mkuu wa mkoa wa Kigoma.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Gerson Msigwa, Andengenye anachukua nafasi ya Emmanuel Maganga aliyestaafu. Mwezi Januari mwaka huu Rais Magufuli alimuondoa kwenye nafasi yake Andengenye, kutokana na kusaini mradi ambao haujapitishwa na Bunge.

Katika sakata hilo, pia aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola naye aliondolewa na nafasi hiyo ilichukuliwa na George Simbachawene. Kwa mujibu wa taarifa hiyo ya Ikulu, pia Rais Magufuli amemteua Dk Philemon Sengati kuwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora, akichukua nafasi ya Aggrey Mwanri ambaye amestaafu.

Taarifa hiyo iliwataja wakuu wa wilaya tisa walioteuliwa na Rais kuwa ni Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza (SACP), Ismail Mlawa anayekuwa Mkuu wa Wilaya ya Kilombero mkoani Morogoro.

Kabla ya uteuzi huo, Mlawa alikuwa Mkuu wa Magereza wa Mkoa wa Morogoro na anachukua nafasi ya James Ihunyo, ambaye amestaafu. Jamila Yusuf ameteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Mpanda mkoani Katavi.

Kabla ya uteuzi huo alikuwa Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Dodoma na anachukua nafasi ya Lilian Matinga, ambaye amestaafu. Rais Magufuli amemteua Martine Ntemo kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kibaha mkoani Pwani.

Kabla ya uteuzi huo, Ntemo alikuwa Mhandisi katika Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano na anachukua nafasi ya Asumpter Mshama, ambaye amestaafu. Mwingine aliyeteuliwa ni Salum Kali anayekuwa Mkuu wa Wilaya ya Magu Mkoani Mwanza na kabla ya uteuzi huo alikuwa Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza na anachukua nafasi ya Dk Philemon Sengati, ambaye ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora. Wilson Shimo ameteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Nyang’wale mkoani Geita na kabla ya uteuzi huo, alikuwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Singida.

Mathias Kahabi ameteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Biharamulo mkoani Kagera akichukua nafasi ya Saada Malunde ambaye amestaafu. Pia Rais Magufuli amemteua Abbas Kayanda kuwa Mkuu wa Wilaya ya Karatu Mkoani Arusha, na kabla ya uteuzi huo alikuwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Karatu na anachukua nafasi ya Theresia Mahongo, ambaye amestaafu.

Lazaro Twange ameteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Babati mkoani Manyara akichukua nafasi ya Elizabeth Kitundu, ambaye amestaafu. Toba Nguvila ameteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Handeni na kabla ya uteuzi huo, alikuwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Longido mkoani Arusha na anachukua nafasi ya Godwin Gondwe, ambaye amehamishwa kituo cha kazi na kuwa Mkuu wa Wilaya ya Temeke mkoani Dar es Salaam. Gondwe anachukua nafasi ya Felix Lyaniva ambaye amestaafu.

Wakati huo huo, Rais Magufuli amemteua Mariam Mmbaga kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu. Kabla ya uteuzi huo, Mmbaga alikuwa Mkurugenzi katika Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi). Mmbaga anachukua nafasi ya Jumanne Sagini. Kwa mujibu wa taarifa hiyo ya Ikulu, uteuzi wa viongozi hao ulianza jana na wateule wote wanatakiwa kuwepo Ikulu, Chamwino mkoani Dodoma Jumatatu saa 4:00 asubuhi.

MGOMBEA urais wa ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

1 Comments

  • avatar
    PASCAL L. MWAWEZA
    17/07/2020

    SAFI SANA MKUU WETU WA NCHI.UBARIKIWE SANA

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi

Magufuli: Nataka kumalizia kazi

masaa 2 yaliyopita Magnus Mahenge, Dodoma

MGOMBEA urais wa ...

Wanawake waihakikishia CCM ushindi

masaa 2 yaliyopita Magnus Mahenge, Dodoma

 

Waziri aagiza mifumo ya fedha ipunguze rushwa

masaa 5 yaliyopita Mwandishi Maalumu, Simiyu

WAZIRI ...