loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Takukuru yaijibu Chadema

TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) imekitaka Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kuendelea kutoa ushirikiano unaopaswa kutolewa kwa Takukuru, kwani kutokufanya hivyo ni kinyume na matakwa ya sheria.

Aidha taasisi hiyo imesema kwamba haielekezwi katika kufanya kazi zake, kwa kuwa ni taasisi huru iliyoundwa kwa mujibu wa sheria za bunge na inajua wajibu wake. Kauli hiyo ilitolewa na Ofisa Uhusiano wa taasisi hiyo, Doreen Kapwani wakati akijibu kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa taasisi hiyo, Brigedia Jenerali John Mbungo, juu ya tuhuma dhidi ya taasisi hiyo, zilizotolewa na Chadema juzi.

“Takukuru imeundwa na kupewa mamlaka ya kutekeleza majukumu yake kwa mujibu wa Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa ya Mwaka 2007 iliyopitishwa na wabunge wakiwemo wa Chadema. Wote wanafahamu lengo na madhumuni ya kuanzishwa chombo hiki pamoja na mamlaka iliyonayo kisheria,” alisema Kapwani.

Juzi Katibu Mkuu wa Chadema, John Mnyika alisema chama chake kinashangazwa na mwenendo wa Takukuru, kutokana na uchunguzi inaoufanya kuhusu chama hicho na kudai ni kinyume na sheria.

Aliitaka taasisi hiyo kueleza rasmi makosa ya chama hicho na si kuchukua kauli za kisiasa na kufanyia uchunguzi. Mwishoni mwa Mei mwaka huu, Takukuru ilianza kuchunguza tuhuma za matumizi mabaya ya fedha za Chadema, ikiwemo wabunge wa chama hicho kukatwa mishahara yao. Baadaye wabunge 69 na viongozi wengine wa chama hicho pamoja na waliowahi kuhudumu kupitia chama hicho, walihojiwa na taasisi hiyo.

“Ni ushauri wa Takukuru kuwa Chadema watulie na wasubiri matokeo ya uchunguzi kwani kupitia uchunguzi wowote unaofanyika, ukweli hujulikana na iwapo hakuna ukweli pia itabainika,” alisema Kapwani.

Kuhusu hoja kwamba taasisi hiyo inatumika kisiasa, alisema haina msingi kwani Takukuru ni chombo huru kinachotekeleza majukumu yake kwa mujibu wa sheria na mamlaka yake ni kuchunguza bila ubaguzi wowote wa rangi, dini, kabila, chama, jinsia, umri wala elimu.

“Ikumbukwe kuwa Chadema wenyewe walisimama bungeni na kutoa malalamiko dhidi ya ubadhirifu wa matumizi ya fedha za michango yao na ni ubadhirifu ni kosa la jinai,” alisisitiza.

Alisema malalamiko hayo, ndio chanzo cha taarifa kwa Takururu, ambapo hata kama suala kama hilo lingetokea kwa chama kingine chochote, taasisi hiyo ingechukua hatua hizo za uchunguzi.

Alisema chombo hicho kina watalaamu waliobobea katika shughuli za kiuchunguzi ; na kamwe hakiwezi kuelekezwa namna ya kufanya uchunguzi wake dhidi ya tuhuma za rushwa na watu inaowachunguza, kwa sababu ni chombo huru kilichopo kwa mujibu wa sheria.

Alieleza kuwa imekuwa ni bahati mbaya, kwamba tuhuma hizo dhidi ya Chadema zinachunguzwa na taasisi hiyo katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu wa viongozi unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu.

“Tuhuma za kijinai zinapotokea haziwezi kuachwa kwa kisingizio cha uchaguzi,” alisema.

TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imetakiwa kuchukua hatua inapoona ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi