loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Tanzania ya pili wabunge wengi wanawake Afrika Mashariki

TANZANIA inashika nafasi ya pili kwa nchi za Afrika Mashariki na nafasi ya 25 duniani, kwa kuwa na asilimia 36.9 ya wanawake wabunge, huku Rwanda ikishika nafasi ya kwanza hadi kidunia kwa kuwa na asilimia 61.3.

Hayo yalisemwa jana na Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), Lilian Liundi wakati wa kikao mkakati wa kujadili ushiriki wa wanawake na vijana na watu wenye ulemavu katika nafasi za maamuzi na uongozi.

Alisema katika Afrika Mashariki, Tanzania ni moja ya nchi zinazofanya vizuri katika ushiriki wa wanawake katika uongozi.

“Kulingana na takwimu za Inter Parliamentary Union (IPU) hadi Januari 2019 Tanzania inashika nafasi ya pili katika nchi za Afrika Mashariki na nafasi ya 25 duniani kwa kuwa na asilimia 36.9 ya wanawake wabunge ambapo Rwanda inashika nafasi ya kwanza hadi kidunia kwa kuwa na na asilimia 61.3.

“Hata hivyo bado hatujaweza kufikia asilimia 50/50 na hivyo hatuna budi kuongeza juhudi katika nafasi za wanawake katika ngazi mbalimbali za maamuzi ili kufikia malengo,” alisema.

Alisema uchaguzi wa mwaka huu, unatoa matumaini makubwa kwamba wanawake vijana na watu wenye elemavu, watajitokeza zaidi kuomba nafasi mbalimbali za uongozi na kuendelea kuiweka nchi katika nafasi nzuri ya utekelezaji wa mikakati ya kikanda na kimataifa.

Alisema Tanzania imefanikiwa kama taifa kwani uchaguzi wa mwaka huu umekuja wakati nchi tayari ilishaweka historia katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015, kwa kumpata kwa mara ya kwanza Makamu wa Rais mwanamke, Samia Suluhu Hassan Pia, alisema katika uchaguzi huo, kulikuwa na mgombea mwanamke katika nafasi ya urais, Anna Mghwira wa chama cha ACTWazalendo.

Pia wanawake wengi walijitokeza kugombea nafasi mbalimbali. Alisema takwimu zinaonesha kuwa hadi Januari 2019, wanawake wakuu duniani walikuwa 10 kati ya 152, sawa na asilimia 6.6 tu, ambapo wanawake wakuu wa serikali walikuwa 10 kati ya 193 sawa na asilimia 5.2.

TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imetakiwa kuchukua hatua inapoona ...

foto
Mwandishi: Sifa Lubasi, Dodoma

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi