loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Serikali yakosa bil 125/- kwa watu 900,000 kukosa hati za ardhi

WAZIRI wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi amesema zaidi ya wamiliki wa ardhi 900,000 nchini, hawajamilikishwa ardhi na kupatiwa hati na hivyo kuisababishia serikali kushindwa kukusanya takribani Sh bilioni 125.

Kufuatia hali hiyo, Lukuvi ameagiza wamiliki wote nchini, wakiwemo zaidi ya 60,000 wa mkoa wa Shinyanga, ambao viwanja vyao vimepimwa na michoro yake kuidhinishwa, waende ofisi za ardhi katika halmashauri za wilaya, kufuatilia hati ili waweze kumilikishwa ndani ya siku tisini

Alibainisha kuwa, mwananchi ambaye atashindwa kwenda kufuatilia hati yake katika kipindi cha siku tisini, atapelekewa stakabadhi ya malipo, ikimtaka alipe kuanzia pale ambapo kiwanja chake kilipimwa na michoro kuidhinishwa. Lukuvi alisema hayo jana mkoani Shinyanga wakati wa uzinduzi ofisi ya ardhi mkoa, ikiwa ni mfululizo wa uzinduzi wa ofisi za ardhi katika mikoa mbalimbali nchini.

“Wale wamiliki ambao watashindwa kufuatilia hati katika kipindi cha siku tisini wataanza kudaiwa kodi ya pango la ardhi kuanzia pale michoro ilipoidhinishwa. Hata kama michoro hiyo iliidhishwa mwaka 1962 ataanza kudaiwa kuanzia hapo, maana itakuwa ni uzembe wake” alisema Lukuvi

Kwa mujibu wa Lukuvi, serikali inataka kila mtanzania apate hati miliki ya ardhi kwa mujibu wa sheria, kwa kuwa serikali inashindwa kukusanya kodi ya ardhi kwa mtu ambaye hana hati.

Aliwataka wamiliki wachukue hati zao ili serikali ipate mapato na kutoa huduma katika sekta mbalimbali, kama vile barabara, maji na hospitali. Zoezi la uzinduzi ofisi za ardhi katika mikoa mbalimbali, limefanyika tayari katika mikoa kumi na linaendelea katika mikoa ya Mara, Geita, Kagera, Lindi na Ruvuma.

TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imetakiwa kuchukua hatua inapoona ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Maalumu, Shinyanga

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi