loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Tani 2.9 za bangi zateketezwa Arusha

MAMLAKA ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Nchini kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi mkoani Arusha, wamefanikiwa kuteketeza zaidi ya tani 2.9 za dawa za kulevya aina ya bangi.

Kufanikiwa kuteketeza kiasi hicho ni kufuatia operesheni maalumu, iliyofanyika katika vijiji vya Engalauni na Lengilong wilayani Arumeru mkoani Arusha. Kaimu Kamishna Jenerali wa mamlaka hiyo, James Kaji alisema hayo alipozungumza na waandishi wa habari wakati wa kazi ya kuteketeza bangi hiyo wilayani Arumeru.

Alisema katika operesheni hiyo iliyofanyika Juni 30 mwaka huu katika vijiji vya Engalauni na Lengilong, walifanikiwa kukamata watu wawili waliokuwa wamehifadhi magunia 65 ya bangi.

Aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni Sauli Mollel (34) aliyekutwa amehifadhi magunia 32 ya bangi. Mwingine ni Losieku Mollel (35) ambaye alikutwa amehifadhi magunia 33 ya bangi.

Wote ni wakazi wa Kitongoji cha Mandeki wilayani humo. Kaimu Kamishina huyo alisema katika operesheni nyingine waliyoifanya Julai 2, mwaka huu wilayani humo, walikamata magunia mengine 75 yaliyokuwa yamehifadhiwa katika boma lililopo Kijiji cha Lengilong na wahusika walifanikiwa kutoroka.

“Watuhumiwa hao bado wanashikiliwa na polisi na watafikishwa mahakamani baada ya uchunguzi kukamilika,” alisema Kaji.

Katika hatua nyingine, Kaji alisema kuwa wanasiasa wamekuwa wakichangia ongezeko la kilimo cha bangi, kwa kuwaaminisha wananchi kwamba serikali ipo mbioni kuruhusu kilimo cha bangi, jambo ambalo si kweli.

Alisema hivi karibuni waliibuka wanasiasa wachache, wakihimiza zao la bangi liruhusiwe kulimwa nchini ili litumike kama dawa ya kutibu magonjwa ya binadamu. Alisema kiwango cha bangi kinachotengeneza dawa ni asilimia mbili tu, hivyo kutokuwa na ulazima wa kuhalalisha zao hilo.

TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imetakiwa kuchukua hatua inapoona ...

foto
Mwandishi: John Mhala, Arusha

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi