loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Wanafunzi DIT watengeneza mashine za kupumulia

WANAFUNZI wa mwaka wa kwanza wa Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam(DIT), wamebuni mashine ya kupumulia (ventilator) kuwasaidia wagonjwa hasa wa maeneo ya vijijini.

Mwanafunzi wa mwaka wa kwanza chuoni hapo anayesoma fani ya vifaa tiba, Innocent Deogras amesema mashine hiyo ina uwezo wa kuzalisha hewa ya Oksijeni na wanafunzi wametumia miezi miwili kuitengeneza.

Alisema hayo alipozungumza na gazeti hili kwenye Maonesho ya 44 ya Kimataifa ya Biashara (DITF), yanayoendelea kwenye Viwanja vya Sabasaba, Dar es Salaam.

Alisema mashine hiyo inatumia mfumo wa umeme wa kawaida au wa jua na inaweza kuhifadhi umeme kwa muda hata kama umeme umekatika, hivyo kuifanya kuwa nzuri zaidi kwenye maeneo yenye changamoto ya umeme hususan vijijini.

Alisema waliwasilisha wazo la mradi kwa uongozi wa chuo hicho na waliwezeshwa kwa vifaa ikiwa pamoja na kupatiwa msimamizi wa mradi ambaye ni Mhadhiri Msadizi, Haji Fimbombaya. Kazi ya mhadhiri huyo ni kuwaongoza hadi mashine hiyo kukamilika.

Deogras alisema kuwa wanafunzi walifikia uamuzi huo, kutokana na upungufu wa mashine za kupumulia katika hospitali mbalimbali nchini, hasa kipindi hiki cha ugonjwa wa Covid 19 unaosababishwa na virusi cha corona.

Alisema kwa sasa mashine hiyo inaweza kufungwa hospitalini na kutumiwa kama mashine nyingine zinazonunuliwa kutoka nje ya nchi. Alibainisha kuwa mashine za aina hiyo kutoka nje ya nchi, zinauzwa kati ya Sh milioni tano hadi 25.

Pia wadau mbalimbali walichanga hadi ujenzi ukafikia hatua ya kuezekwa ...

foto
Mwandishi: Evance Ng’ingo

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi