loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Uchelewaji kwenda kliniki wasababisha vifo vya ‘vichanga’ 322 Shinyanga

WATOTO wachanga 322 wamefariki mkoani Shinyanga katika kipindi cha miezi sita kuanzia Januari hadi Juni mwaka huu, kutokana na wajawazito kuchelewa kuanza kliniki.

Hali hiyo imesababisha wapate matatizo ya kiafya, ikiwemo kifafa cha mimba na kutokwa na damu nyingi. Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga, Albert Msovela alisema hayo juzi wakati akifungua kikao kazi cha uhamasishaji huduma za afya ya uzazi na mtoto. Kikao hicho kilihusisha makundi mbalimbali ya kijamii. Alisema kuwa idadi hiyo ni kubwa na inasikitisha.

Mbali na vifo vya watoto wachanga, pia kuna vifo 121 vya wajawazito vilivyotokana na uzazi kuanzia mwaka 2018 hadi Juni 2020. Vifo hivyo vinachangiwa na wajawazito kupata matatizo ya kupasuka kwa mji wa mimba, kifafa cha mimba na kutokwa damu nyingi.

“Mwaka 2018 tulikuwa na vifo vya wajawazito 56, mwaka 2019 vifo 50 na Januari hadi Juni 2020 vimetokea vifo 15, hii idadi ni kubwa, pamoja na changamoto ya ugonjwa wa Covid-19 ambao unaendelea kupungua kwa kasi bado wanatakiwa kuimarisha huduma na kuhimiza wajawazito kuwahi kupata huduma,” alisema Msovela.

Mratibu wa Elimu ya Afya kwa Umma mkoa wa Shinyanga, Halima Hamisi aliitaka jamii kuacha tabia ya kuwapa dawa za kuongeza uchungu wajawazito, kutokana na kuwasababishia madhara makubwa, ikiwemo kupoteza maisha mama na mtoto na wengine kupata kifafa cha mimba.

Alisema wajawazito kuchelewa kuanza kliniki chini ya wiki 12 na kutojifungulia vtuo vya kutolea huduma, lishe duni, upungufu wa damu ni mambo ambayo yamekuwa yakichangia vifo kutokea.

Alieleza kuwa mwezi Oktoba hadi Desemba mwaka jana, wajawazito 18,500 walitarajiwa kufika kliniki lakini waliofika ni 15,900 tu. Mwaka huu kuanzia Januari hadi Machi lengo lilikuwa wajawazito 19,000, lakini waliofika kliniki ni 17,000, kitendo ambacho kitachangia kuendelea kuwepo vifo.

Pia wadau mbalimbali walichanga hadi ujenzi ukafikia hatua ya kuezekwa ...

foto
Mwandishi: Kareny Masasy, Shinyanga

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi