loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

China, Tanzania zilivyoungana kukabiliana na Covid-19

HIVI karibuni gazeti moja la kila siku liliandika habari yenye lengo la kuvuruga uhusiano mzuri kati ya China na Afrika ikiituhumu kuwa chanjo dhidi ya virusi vya corona na kwamba, China ilichelewa kutoa habari za maambukizi ya mlipuko huo.

Ukiyatafakari kwa makini madai hayo, utabaini yanalenga kuharibu uhusiano mzuri uliopo kati ya Afrika na China na pia, kupunguza ushawishi wa China barani Afrika.

Lawama hizo zinazotokana na China kuwa nchi ya kwanza kukumbwa na mlipuko wa Covid-19 mwishoni mwa mwaka jana kabla ya kusambaa katika nchi nyingine duniani, haziingii akilini kutokana na ubaya wa lengo.

Mwandishi katika makala hiyo anawachukulia raia wa China kama chanzo cha virusi vya corona hali inayoleta hofu na ubaguzi dhidi ya Wachina pamoja na Waasia popote walipo duniani.

Hoja ya mwandishi huyo haikuishia kuilaumu China na wananchi wake pekee, bali pia alizungumzia Bara la Afrika na kusema kwa kuwa halijaendelea kiteknolojia, litaathirika zaidi na mlipuko huo.

Maneno yote yaliyoandikwa ya kubeza uwezo wa nchi za Afrika kukabiliana na ugonjwa huo, ukiyaangalia utaona ni siasa yenye lengo la kusambaza uongo na kupunguza uwezo wa ndani kukabiliana na maambukizi hayo kwa kusababisha kutojiamini.

Madai ya kuficha ukweli Ingawa kuna wachambuzi na wanasiasa wanaodai kwamba China imeficha ukweli kuhusu chanzo cha virusi vya corona na kushindwa kuzuia maambukizi kuenea zaidi, ukweli ni kuwa China ilitimiza wajibu wake kwa kasi kubwa baada ya kubaini uwapo wa mlipuko huo.

Kwa mujibu wa taarifa ya Shirika la Afya Duniani (WHO), China ilitoa taarifa kwa shirika hilo mapema mwanzoni mwa mwezi Januari 2020. WHO ilichukua hatua za haraka na kuunda Tume maalumu ya kukabiliana na Covid-19 mara moja.

Taarifa za WHO zinaonesha kuwa, taarifa zilizotolewa na China kwa wakati zimesaidia kuzuia idadi kubwa ya watu kupata maambukizi. Jarida la Kitaaluma la Sayansi nalo lilikiri hatua za haraka za China kupunguza usambaaji wa virusi hivyo kwa nchi nyingine kutokana na kujikinga.

Kuhusu “chanzo cha virusi vya corona”, ijapokuwa China imeshutumiwa kutengeneza virusi vya corona katika maabara kwa kudhamiria, Mkurugenzi wa Ofisi ya Intelejensia ya Marekani anasema wamechunguza kwa kina na kuungana na wanasayansi wengine kuwa chanzo cha ugonjwa huo ni cha kiasili wala siyo kutengenezwa kwa kudhamiria.

Tanzania, China vita ya corona Februari 3 mwaka huu, wakati maradhi ya Covid-19 yalipolipuka kwa nguvu nchini China, Rais wa Tanzania, John Magufuli alituma salamu za rambirambi kwa Rais Xi Jinping kuhusu janga hilo la kutishia.

Katika salamu zake, Rais Magufuli alisifu hatua za haraka na zenye nguvu zilizochukuliwa na serikali ya China na ujasiri uliooneshwa na watu wa China. Rais Magufuli alisema Tanzania itasimama pamoja na China ili kulishinda janga hilo kwa haraka.

Wakati nchi za Tanzania na China zikiwa zinakabiliwa na janga hilo la aina moja, China imetoa misaada kwa Tanzania bila kusita. Hadi Mei 16 mwaka huu, China imetoa msaada wa vyombo vya kujikinga na virusi vya corona kwa kila njia.

Kwa mfano, Serikali ya China imetoa vifaa tiba kwa Zanzibar zikiwemo barakoa 2,000 za aina ya KN95, barakoa 10,000 za upasuaji, nguo 2,000 za kujikinga dhidi ya virusi, jozi 10,000 za glovu, jozi 2,000 za miwani ya usalama, jozi 10,000 za vifuniko vya miguu, na vipimajoto 500 vya infrared.

Vifaa vya matibabu vilivyotolewa na Shirika la Mayun Foundations na Shirika la Alibaba Foundations ni pamoja na vitendanishi vya kupimia virusi, mashine za kupumulia, barakoa na glavu, nguo za kujikinga na kadhalika.

Zaidi ya hayo, Ubalozi wa China nchini Tanzania na kampuni za China nchini Tanzania pia zimetoa misaada mbalimbali, zikichangia vifaa vya matibabu na vifaa vya ujenzi vinavyotumika kujenga karantini za kujitenga. Michango hiyo imesaidia Tanzania kusuluhisha ukosefu wa vifaa tiba.

Licha ya hayo, ili kutoa misaada ya kidaktari na kiufundi, Wizara ya Mambo ya Nje ya China na Kamati ya Kitaifa ya Afya ya China ziliandaa mikutano mitatu kwa njia ya mtandao juu ya jinsi China ilivyodhibiti na kujikinga na maradhi ya Covid-19. Katika mikutano hiyo, wataalamu wa China walishirikiana na maafisa wa Afrika juu ya namna ya kuzuia virusi na matibabu ya ugonjwa. China itaendelea kuwapa Waafrika uzoefu na misaada ya kupambana na maradhi ya Corona.

Ubora wa vifaatiba Vifaa vilivyotolewa na Serikali ya China vyote vimezalishwa kwa kufuata kanuni za utengenezaji na vimekidhi viwango vya ubora wa kimataifa. Vifaa kama barakoa na nguo za kujikinga vimesambazwa kwa madaktari na wauguzi wa hospitali nchini Tanzania na kufikia sasa, hakuna mtu yeyote aliyelalamika juu ya uhafifu wa vifaa vilivyotolewa na China.

Visa vilivyosababisha madai hayo ya “uhafifu wa vifaa” ni pamoja na viwango tofauti vya ukaguzi wa Shirika la Ubora wa Viwango Duniani (ISO). Kwa mfano, watu wa nchi za Ulaya wanatumia barakoa za FFP1 huku watu wa China wanatumia barakoa za KN95, ingawa barakoa hizo ni za aina tofauti, zote zinaweza kuzuia virusi vya corona kwa ufanisi mkubwa.

Misaada kwa nchi za Afrika Watu wengine wametoa hoja kwamba China inazisaidia nchi za Afrika maana inataka kunyang’anya maliasili za Afrika. Hii siyo kweli. China ilijenga uhusiano wa kirafiki na nchi nyingi za Afrika tangu zilipojipatia uhuru, uhusiano na ushirikiano baina ya nchi hizi unaendelea vizuri mpaka leo.

Tanzania na China ni kama hivyo, zina historia za aina moja, tena zina urafiki wa tangu zamani sana. Wakati maradhi ya Covid-19 yalipolipuka nchini China, viongozi wa Tanzania pia waliitumia China salamu za pole na rambirambi. Wakati wote pande hizo mbili zinasaidiana na kuunga mkono katika jukwaa la kimataifa. Hivyo ni lazima China irudishe hisani na misaada Tanzania inapokabiliwa na shida.

Kwa sababu China ni nchi ya kwanza kukumbwa na janga la corona, Wachina wanahurumia sana nchi nyingine zinazokabiliwa na tatizo hili. Sasa virusi vya corona vimedhibitiwa kwa ufanisi mkubwa nchini China, hivyo serikali ya China iko tayari kubadilishana uzoefu na nchi nyingine zinazohitaji misaada.

Kuishinda corona Zaidi ya misaada inayotolewa na China, nchini Tanzania kuna Wachina wengi wanaoishi nao wote wanashirikiana na Watanzania ili kuishinda corona kwa haraka.

Ingawa shule na vyuo nchini Tanzania vilifungwa na kufunguliwa siku za karibuni kwa sababu ya ugonjwa, walimu wa Taasisi ya Confucius ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (CIUDSM) waliendelea kufundisha lugha ya Kichina kwa wanafunzi kwa njia ya mtandao.

Mwalimu Zhang Yinfeng ni mmojawapo wa walimu wa kujitolea katika CIUDSM. Huu ni mwaka wake wa pili kufundisha Kichina hapa Tanzania. Anasema kwamba, “tunafundisha lugha ya Kichina wakati huu wa corona si kwa lengo la kujifunza lugha tu, bali pia tunawapa wanafunzi moyo ili kuishinda corona kwa haraka.”

“Tunatumaini wanafunzi wote wako salama katika kipindi hiki kigumu. Hivyo wakati tunapowafundisha ujuzi wa Kichina, pia tunawaambia namna ya kujikinga na ugonjwa.”

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimembariki Samia Suluhu Hassan kuwa mgombea ...

foto
Mwandishi: Ning Yi

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi