loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Castico ataja kiini kushamiri kwa udhalilishaji kijinsia

WAZIRI wa Kazi, Uwezeshaji, Wanawake, Watoto na Wazee, Moudline Castico amesema matukio ya udhalilishaji wa kijinsia, yameshamiri Zanzibar kwa sababu ya jamii kuoneana “muhali” na kukataa kutoa ushahidi mahakamani.

Castico alisema hayo wakati akikabidhi tuzo kwa waandishi wa Jumuiya ya Waandishi wa Habari za Maendeleo (WAHAMAZA), ambao walishiriki katika mradi wa kuandika habari za changamoto zinazowakabili wanawake na watoto katika kupata haki zao msingi.

Alisema wapo baadhi ya wananchi, hawatoi ushirikiano wakati wa kutafuta ufumbuzi wa kesi za udhalilishaji wa kijinsia na matokeo yake ni kufutwa kwa kesi hizo mahakamani.

“Tunazo sheria nzuri za haki ya watoto pamoja na kupambana na vitendo vya udhalilishaji wa kijinsia lakini tunakabiliwa na ‘muhali’ ikiwemo kukataa kutoa ushahidi mahakamani,” alisema.

Aliwataka waandishi wa habari kuendelea na kuzipatia ufumbuzi changamoto mbalimbali, zinazowakabili wanawake na watoto ambazo ni kikwazo katika kuyafikia maendeleo kwa makundi hayo ikiwemo sekta ya elimu.

“Waandishi wa habari fanyeni kazi ya kuzipatia ufumbuzi changamoto zinazowakabili wanawake na watoto....tutatoa ushirikiano katika suala hili,” alisema.

Katibu wa WAHAMAZA, Salma Said alisema mafanikio makubwa yamepatikana katika mradi wa kuandika habari za maendeleo vijijini kwa ajili ya kufichuwa matukio ya udhalilishaji kwa watoto na kuona wanapata haki zao za msingi.

“Matatizo yanayowakabili watoto ni mengi .... juhudi zaidi zinahitajika kuona kwamba watoto wanaondokana na matatizo na changamoto ambazo ni kikwazo katika kuyafikiya malengo ikiwemo elimu,” alisema.

Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa Linaloshughulikia Watoto (UNICEF) anayeshughulikia miradi, Maha Damaj aliwataka waandishi wa habari kutekeleza majukumu yao na kufanya uchunguzi wa matukio ya vitendo vya udhalilishaji wa kijinsia, ambavyo hurudisha nyuma maendeleo ya watoto na ukuaji wao kwa ujumla.

IDADI ya watalii kutoka ...

foto
Mwandishi: Khatib Suleiman

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi