loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Msongamano wa wanafunzi wajitokeza baadhi ya shule

WAKATI shule za msingi za Unguja na Pemba zikifunguliwa na kuruhusu wanafunzi kuanza masomo kwa kuzingatia masharti ya afya ya kujikinga na virusi vya corona, tatizo la msongamano na wanafunzi limejitokeza kwa baadhi ya shule.

Uchunguzi uliofanywa na gazeti hili, umegundua idadi ya wanafunzi wanaotakiwa kusoma katika darasa moja ni 40, lakini baadhi ya madarasa wapo zaidi ya wanafunzi 90. Mwalimu katika Shule ya Mto Pepo aliyejitambulisha kwa jina la Iddi Ali, alisema shule yao inakabiliwa na uhaba wa madarasa kwa hivyo darasa moja wanasoma zaidi ya wanafunzi 100.

“Masharti yaliyowekwa na Wizara ya Elimu kila darasa moja linatakiwa wawepo wanafunzi 40... lakini kwa bahati mbaya idadi ya wanafunzi katika darasa moja ni zaidi ya wanafunzi mia moja,” alisema.

Alisema tayari wamewaita wazazi wa wanafunzi katika shule hiyo, ikiwemo kuanzisha utaratibu wa kuwepo vipindi vya nyakati za asubuhi na mchana kwa ajili ya kupokea wanafunzi.

Mkurugenzi wa Elimu ya Msingi, Safia Rijali alikiri kuwepo kwa tatizo la msongamano wa wanafunzi katika baadhi ya shule nyingi, ikiwemo za mjini, licha ya kuwepo kwa shule za ghorofa zilizofunguliwa hivi karibuni.

Alisema Wizara ya Elimu inalifahamu tatizo la wingi wa wanafunzi unaosababishwa na msongamano mkubwa wa wanafunzi na suala hilo litapatiwa ufumbuzi.

“Shule zetu nyingi zinakabiliwa na msongamano mkubwa wa wanafunzi kiasi ya darasa moja kusoma wanafunzi mia moja kinyume na maelekezo ya kuwepo wanafunzi 40...tutalifanyia kazi na kulipatia ufumbuzi,” alisema.

Pia wadau mbalimbali walichanga hadi ujenzi ukafikia hatua ya kuezekwa ...

foto
Mwandishi: Khatib Suleiman

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi