loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

YANGA YAIFUATA BIASHARA

MABINGWA wa kihistoria, Yanga wametua Musoma, Mara, huku kocha wao akisema kuwa Benard Morrison hayumo katika mpango wake wa mchezo wa kesho dhidi ya Biashara United.

Yanga jana mchana ilitua Mwanza kwa ndege kabla ya kupanda basi na kwenda Musoma, Mara, ambako kesho watacheza mchezo huo wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Kocha wa Yanga, Luc Eymael Morrison alisema jana kuwa kikosi chao kimekwenda Musoma pamoja na Morrison kurejea kambini, lakini hatamtumia katika mchezo huo kwenye Uwanja wa Karume mjini Musoma.

Kikosi hicho kina morali baada ya kutoka kufuzu nusu fainali ya Kombe la Shirikisho dhidi ya Kagera Sugar kwa ushindi wa mabao 2-1 uliochezwa hivi karibuni kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Yanga imedhamiria kushinda mchezo huo sambamba na mchezo wa ligi wa Julai 9, dhidi ya Kagera Sugar kabla ya kurudi Dar es Salaam kujiandaa na mchezo wa nusu fainali dhidi ya Simba utakaochezwa Julai 12, mwaka huu.

Eymael aliliambia gazeti hili kuwa mchezo wa kesho ni muhimu kwao kupata pointi tatu ili kuendelea kujiimarisha katika nafasi ya pili.

“Lengo letu ni kupata pointi tatu, tumedhamiria kupambana na kufanya vizuri, tunajua mechi haitakuwa rahisi kwasababu Biashara ni moja ya timu nzuri na nimefuatilia matokeo yake hivi karibuni wamekuwa bora, hasa kwenye uwanja wao ila sisi tunajua tunachokitaka,”alisema.

Mchezaji aliyekosekana kwa muda mrefu Bernard Morrison alianza mazoezi, lakini kwa mujibu wa Eymael hatokuwa sehemu ya mchezo wa kesho bali aliahidi kucheza mchezo wa nusu fainali wa FA dhidi ya Simba.

Morrison amekuwa kwenye mvutano na klabu hiyo kuhusu mkataba wake akidaiwa kutokuwa na nidhamu baada ya kuwahi kutoroka mazoezini mara kadhaa kabla ya michezo iliyopita, huku akihusishwa kuwa anataka kwenda upande wa pili wa watani zao wa jadi.

Aidha, mshambuliaji wa Yanga Ditram Nchimbi alizungumzia mechi dhidi ya Biashara na Kagera kuwa wanahitaji kushinda ili wakae vizuri kisaikolijia kujiandaa na Simba.

“Mwalimu amefanyia kazi mapungufu tumeshajiandaa kupata pointi sita au nne kwetu itakuwa furaha, kusudi kutimiza lengo la kubakia nafasi ya pili, lakini pia kuongeza morali kuelekea mchezo wa nusu fainali wa FA dhidi ya Simba,”alisema.

Mara ya mwisho Yanga kukutana na Biashara ilikuwa kwenye mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu, ambapo walishinda bao 1-0 Dar es Salaam, hivyo Biashara wana deni la kulipa.

foto
Mwandishi: Grace Mkojera

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi

Kila mchezaji wa kigeni mil 4

masaa 21 yaliyopita Rahel Pallangyo

KLABU ya ...

Kila mchezaji wa kigeni mil 4

masaa 21 yaliyopita Rahel Pallangyo

KLABU ya ...

Simba yamuwekea kizuizi Senzo Yanga

masaa 22 yaliyopita Mohammed Mdose

SIKU moja ...