loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Washiriki Nanenane kula, kunywa korosho

WASHIRIKI wa Maonesho ya Nanenane Kanda ya Kusini mwaka huu 2020 katika Viwanja vya Ngongo mkoani Lindi, watapata burudani ya pekee, ambayo pamoja na kujifunza teknolojia mbalimbali katika sekta ya kilimo na ufugaji, watapata nafasi ya kula na kuinywa korosho.

Mkurugenzi Tari Naliendele, Dk Fortunatus Kapinga amesema hayo alipozungumza baada ya kikao cha kamati ya maandalizi ya maonesho hayo, kilichokusanya wadau kutoka mikoa ya Kusini.

Alisema kwamba maonesho ya mwaka huu, yametengwa kuwa na siku maalumu ya korosho, ili kuhamasisha wananchi kuhusiana na zao hilo.

Alisema washiriki watapewa taarifa za zao hilo na tekenolojia yake, ikiwemo kilimo chake na pia wanatapata nafasi ya kula korosho zenyewe, maziwa ya korosho, juisi ya korosho na milo mbalimbali iliyochanganywa na korosho.

Alisema lengo kuu ni kuwafanya wawekezaji katika sekta hiyo, kutambua bidhaa zaidi ya korosho ya kutafunwa.

Alisema korosho inaweza kutengenezwa maziwa, huku bibo lake likiweza kutengenezwa juisi iliyojaa vitamini nyingi na pombe aina ya mvinyo.

Dk Kapinga alisema kuwa Tari Naliendele ambayo inafanya shughuli zake mwaka mzima katika viwanja hivyo vya Ngongo, imejiandaa vyema kufundisha na pia kubadilisha mtazamo kuhusu zao la korosho, ili wawekezaji waweze kuwekeza katika utengenezaji wa bidhaa mbalimbali.

Katika mkutano huo wa wadau, uliofanyika katika viwanja hivyo chini ya Katibu Tawala Mkoa wa Lindi, Rehema Madenge pamoja na Katibu Tawala Mkoa wa Mtwara, Alphayo Kidata, iliamriwa kwamba maonesho hayo yataanza kwa nguvu Agosti Mosi.

Rehema aliwataka wadau, taasisi mbalimbali, mashirika, wakulima na mamlaka za serikali za mitaa mkoa wa Lindi na Mtwara, kukamilisha michango yao na kwa muda unaotakiwa. Ilielezwa katika kikao hicho kuwa Agosti 6 mwaka huu, itakuwa siku ya wadau wa korosho.

Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Newala, Mussa Chimae, alisema kuwa wilaya yake itakuja na mambo mapya katika maonesho hayo, yakiwemo tuiba lishe kutoka kwa wakulima na wajariamali wa wilaya hiyo.

Pia Mkurugenzi wa Kilwa, Renatus Mchau alisema kwamba wilaya ya Kilw aitaleta vitu vingi ikiwamo bidhaa mbalimbnali za Kilimo na ufugaji na pia utalii.

Awali katika mkutano huo Katibu Tawala Lindi, Rehema Madenge aliwakumbusha wadau kukamilisha maandalizi yao na pia watu wamaji (RUWASA) kuhakikisha wana maji muda wote.

“Tumia teknolojia za kilimo na utawala bora kwa ukuaji wa ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Maalumu,Lindi

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi