loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Wazabuni Bwawa la Nyerere kufuatiliwa

WIZARA ya Viwanda na Biashara itafuatilia wamiliki wote wa viwanda, waliopewa zabuni ya kusambaza vifaa vya ujenzi katika Mradi wa Kufua Umeme wa Maji wa Julius Nyerere (JNHPP) wilayani Rufi ji mkoani Pwani.

Itafanya hivyo ili kuhakikisha kuwa wanazalisha vifaa vinavyokidhi ubora vya mradi huo, unaogharimu fedha nyingi serikali.

Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Stella Manyanya alisema hayo hivi karibuni alipotembelea mradi huo akiwa na Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu.

Katika ziara hiyo, walipitishwa eneo la mitambo ya kusaga mawe na kutengeneza zege, handaki la kuchepusha maji na sehemu ya kuvunia maji katika mradi huo.

Manyanya alisema mradi huo ni miongoni mwa miradi mikubwa nchini, ambayo ujenzi wake umehusisha wadau mbalimbali kutoka taasisi za serikali na sekta binafsi.

Hivyo, alisema ni wajibu kwa wenye viwanda kutoa malighafi zenye ubora kwa ajili ya mradi huo.

Pia wadau mbalimbali walichanga hadi ujenzi ukafikia hatua ya kuezekwa ...

foto
Mwandishi: John Nditi, Morogoro

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi