loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Yanga, Azam kazi ipo leo

BAADA ya bingwa wa Ligi Kuu soka Tanzania Bara Simba kufanikiwa kutetea taji, vita imehamia kwa Yanga na Azam zikigombea namba mbili, ambapo leo wote watashuka dimbani kwenye viwanja tofauti kutafuta pointi tatu muhimu.

Simba imebakisha mechi za kukamilisha ratiba, na leo itakuwa ugenini dhidi ya Ndanda, Yanga nayo ikiwa ugenini dhidi ya Biashara United na Azam nyumbani dhidi ya Singida United. Katika vita ya nafasi ya pili, Yanga na Azam zinatazamana na kila mmoja akimuombea mwenzake mabaya ili atateleza na kushuka chini na mwenzake apande juu. Mchezo wake wa leo unaweza kuwa mgumu kutokana na kasi ya Biashara msimu huu kwenye uwanja wake wa nyumbani imejitahidi kupata matokeo mazuri katika baadhi ya mechi zake zilizopita. Yanga ilikutana na Biashara mara tatu na kati ya hizo, imeshinda michezo miwili ikiwa kwenye uwanja wa nyumbani na iliwahi kupoteza kwenye Uwanja wa Karume, Musoma msimu uliopita mchezo mmoja.

Katika michezo miwili iliyopita, mabingwa hao wa kihistoria wamekuwa hawako vizuri katika safu ya ulinzi yote wameruhusu mabao kwa kushinda mabao 3-2 dhidi ya Ndanda na sare ya 2-2 dhidi ya Namungo na wapinzani hutangulia kufunga kisha wao huyarudisha.

Safu yao ya ushambuliaji imekuwa ikisuasua kwa kushindwa kutumia nafasi nyingi wanazopata.

Wasiporekebisha makosa yao wanaweza kuadhibiwa na Biashara, ambao licha ya kushika nafasi za kati kwa pointi 44 wamekuwa wakijitahidi hasa wanapokuwa nyumbani. Mechi zao mbili zilizopita walishinda 4-0 dhidi ya KMC na kutoka sare ya bao 1-1 dhidi ya Azam FC.

Yeyote ana nafasi ya kushinda kulingana na alivyojipanga dhidi ya mchezo huo.

Azam FC huenda wakatumia uwanja wa nyumbani kutafuta matokeo baada ya kushindwa kupata matokeo katika mechi mbili za mikoani dhidi ya Biashara waliotoka sare ya bao 1-1 na kupoteza kwa Kagera Sugar bao 1-0 yaliyowashusha hadi nafasi ya tatu.

Singida inayoshika mkia kwa pointi 15 hata ijitahidi vipi bado mambo sio shwari itaendelea kusalia mwishoni hivyo, kazi kubwa ipo kwa Azam ili iweze kurudi nafasi ya pili, huku ikiiombea Yanga ifungwe.

Simba inatarajiwa kucheza na Ndanda. Inaweza kuhitaji matokeo kwa ajili ya kulinda heshima lakini zaidi mwenye presha ni Ndanda aliyeko kwenye mstari wa kushuka daraja akishika nafasi ya 17 kwa pointi 35 anayehitaji kupambana kujinasua.

Alliance itachuana na Mtibwa Sugar na zote zinahitaji matokeo, wenyeji wanashika nafasi ya 16 kwa pointi 36 akifungwa atazidi kuzama na wageni hao wa Morogoro nafasi ya 13 kwa pointi 37 wanahitaji kupanda juu la sivyo, wanaweza kurudi chini.

Mbeya City itakuwa mwenyeji wa Coastal Union kwenye Uwanja wa Sokoine, wanahitaji kujinasua katika nafasi ya 18 walipo kwa pointi 33 iwapo wakipoteza watajididimiza tofauti na wenzao wanaotafuta matokeo kujiimarisha nafasi za juu.

foto
Mwandishi: Grace Mkojera

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi

Kila mchezaji wa kigeni mil 4

masaa 18 yaliyopita Rahel Pallangyo

KLABU ya ...

Kila mchezaji wa kigeni mil 4

masaa 18 yaliyopita Rahel Pallangyo

KLABU ya ...

Simba yamuwekea kizuizi Senzo Yanga

masaa 19 yaliyopita Mohammed Mdose

SIKU moja ...