loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Tshishimbi- Nasubiri kusaini mkataba Yanga

NAHODHA wa timu ya Yanga Kabamba Tshishimbi amewataka mashabiki wa timu hiyo kuwaunga mkono wachezaji badala ya kuwakejeli.

Tshishimbi alisema hayo jana wakati alipotembelea banda la klabu hiyo lililopo katika maonesho ya 44 ya kimataifa ya biashara yanayoendelea katika viwanja vya sabasaba, Dar es Salaam.

Alimtolea mfano mshambuliaji David Molinga namna mashabiki walivyomkejeli hivi karibuni alipokuwa hafanyi vizuri na kutaka tabia hiyo ikomeshwe na badala yake mashabiki wawe mstari wa mbele kuwaunga mkono.

Aliwataka mashabiki kujenga utaratibu wa kusikiliza maelezo ya timu kutoka kwa Kocha Mkuu wa klabu au viongozi wengine badala ya habari za mitandaoni, huku akiwataka kufahamu kuwa mchezaji Morrison bado ni mali ya Yanga tofauti na inavyoelezwa.

Kuhusiana na hali yake ya kiafya kwa sasa alibainisha kuwa yupo salama na anaweza kucheza kwenye mchezo wa Julai 12 dhidi ya Simba kama kocha akimpanga.

Alisema ameshazungumza na klabu ya Yanga kuhusu kuongeza muda na kwa sasa anasubiria kusaini mkataba huo.

“Ninachoweza kusema ni kuwa mashabiki wafike katika banda hili kujua mambo mengi kuhusiana na Yanga na sio kama ilivyo kwa sasa wanakuwa wanasikiliza maoni ya mitandaoni yenye kulenga kutochinganisha wachezaji na viongozi”alisema.

Kwa upande wake Mhamasishaji wa klabu hiyo, Antonio Nugaz alisema klabu hiyo imejipanga kushinda mchezo wake dhidi ya Simba na kuwa itashinda kwa mabao matatu.

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi

Kila mchezaji wa kigeni mil 4

masaa 19 yaliyopita Rahel Pallangyo

KLABU ya ...

Kila mchezaji wa kigeni mil 4

masaa 19 yaliyopita Rahel Pallangyo

KLABU ya ...

Simba yamuwekea kizuizi Senzo Yanga

masaa 19 yaliyopita Mohammed Mdose

SIKU moja ...