loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Namungo, KMC zafanya kweli

TIMU ya soka ya Namungo imepata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya JKT Tanzania katika mchezo wake wa jana uliochezwa kwenye Uwanja wa Majaliwa, Lindi.

Ushindi huo unaendelea kuibakisha Namungo katika nafasi ya tatu ikifikisha pointi 59 sawa na za Azam FC zikitofautiana mabao ya kufunga na kufungwa. Azam wenyewe wanacheza mchezo wao lao.

Aidha, KMC ilishinda mabao 3-2 dhidi ya Mwadui katika mchezo uliochezwa kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi.

Mwadui ndio iliyokuwa ya kwanza kupata bao la uongozi kisha KMC ilisawazisha na kufunga ya ushindi.

Ushindi wa timu hiyo ya Kinondoni umeitoa katika mstari wa hatari kutoka nafasi ya 15 na kupanda nafasi mbili juu hadi ya 13 na kufikisha pointi 40.

Mchezo mwingine, Mbao ilishinda nyumbani mabao 2-0 dhidi ya Lipuli na kufikisha jumla ya pointi 32 ila ikiendelea kushika nafasi ya pili kutoka mwisho, huku Lipuli ikishuka nafasi moja chini kutoka 14 hadi 15.

Kagera Sugar ikiwa nyumbani ililazimishwa sare ya bao 1-1 dhidi ya Ruvu Shooting na Tanzania Prisons ikisuluhu dhidi ya Polisi Tanzania.

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi

Kila mchezaji wa kigeni mil 4

masaa 17 yaliyopita Rahel Pallangyo

KLABU ya ...

Kila mchezaji wa kigeni mil 4

masaa 17 yaliyopita Rahel Pallangyo

KLABU ya ...

Simba yamuwekea kizuizi Senzo Yanga

masaa 18 yaliyopita Mohammed Mdose

SIKU moja ...