loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Filbert Bayi watamba majaribio riadha

MKOA wa Pwani umeanza kwa kishindo maandalizi ya kushiriki mashindano ya taifa ya riadha yatakayofanyika Septemba mwaka huu, baada ya kung’ara katika mbio za majaribio zilizofanyika kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam jana.

Katika majaribio hayo, wachezaji wa Pwani wengi wao kutoka Shule za Filbert Bayi (FBS) walitamba karibu katika mbio zote kwa kushika nafasi za juu na kuubeba mkoa wa Pwani katika majaribio hayo yaliyoshirikisha pia wanariadha wa mkoa wa Dar es Salaam.

Katibu Mkuu wa Chama cha Riadha Mkoa wa Dar es Salaam (DAA), Lucas Nkungu alisema jana kuwa lengo la mashindano hayo ni kuwapima wanariadha wa Pwani na Dar es Salaam kwa ajili ya kushiriki mashindano ya taifa yatakayofanyika Septemba 5 na 6 kwenye Uwanja wa Taifa na kushiriki mikoa yote ya Tanzania Bara na Zanzibar.

Alisema huo ni mwanzo kwani watakuwa na jumla ya mashindano matatu ya majaribio kabla ya kufanyika kwa mashindano hayo ya taifa, ambayo hayajafanyika kwa miaka mingi bila sababu za msingi.

Katika mbio za meta 400 wanawake, Regina Deugratius, Gaudensia Maneno na Pili Mipawa wote kutoka FBS walishika nafasi tatu za kwanza kwa kutumia dakika 58:43, 58:7 na 60:00 huku wanaume wao, Benedicto Mathias na Matiku Sarya walimaliza katika nafasi mbili za kwanza kwa kutumia dakika 49:70 na 51:29 huku mshindi watatu ni John Siuwa wa shule ya Mlimani aliyekimbia kwa dakika 51:53.

Katika mbio za meta 100 kwa wasichana, Shija Donald na Siwema Julius wote wa FBS walimaliza katika nafasi mbili za kwanza kwa kutumia dakika 13:17 na 13:45 huku Nuru Nasra Khamu wa Mlimani alimaliza watatu kwa kutumia dakika 15:12 huku kwa wavulana katika mbio kama hizo kwa wavulana, Mlimani walitamba kwa kushika nafasi mbili za kwanza huku Yombo wakitamba katika mbio za watoto wadogo wavulana waliokimbia meta 800 huku Daud Omari akishinda kwa dakika 12:50.

Kwa wasichana walikimbia katika mbio za meta 800, Regina Deogratius na Gaudencia Maneno walimaliza wa kwanza na pili katika mbio hizo.

Kocha wa riadha wa FBS Ron Davis alisema kuwa mashindano hayo yalikuwa mazuri ya yenye kutia moyo hasa ukizingatia kuwa wanariadha wengi pamoja na udogo wao, baso wamefanya vizuri kwa upande wa muda.

Alisema kuwa hiyo inadhihirisha kuwa wataendelea hivyo katika jaribio la tatu na nne, basi hakuna ubishi kuwa wanariadha walioshiriki mashindano hayo ya majaribio, bila shaka watafanya vizuri katika mashindano ya taifa Septemba.

Naye muandaa wa jaribio hilo, Bayi aliwataka wanariadha kutoka Pwani na Dar es Salaam kujitokeza kwa wingi ili kujiandaa vizuri kwa mashindano hayo ya taifa ili kuwa na muda mzuri. Lengo ni kuhakikisha wanariadha wanajiandaa vizuri kwa mashindano ya taifa kwa kutoa upinzani mkali usiotarajiwa.

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi

Kila mchezaji wa kigeni mil 4

masaa 18 yaliyopita Rahel Pallangyo

KLABU ya ...

Kila mchezaji wa kigeni mil 4

masaa 18 yaliyopita Rahel Pallangyo

KLABU ya ...

Simba yamuwekea kizuizi Senzo Yanga

masaa 19 yaliyopita Mohammed Mdose

SIKU moja ...