loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

NCBA Bank Tanzania yateua Mkurugenzi  wapya

BENKI za NIC Tanzania na CBA wapo mbioni kumalizia uunganaji wa taasisi zao na kuanza kutoa huduma zao kama NCBA Bank Tanzania Ltd.

Aidha wajumbe wa bodi teule wamemteua Margaret Karume kuwa Mkurugenzi na Afisa Mkuu Mtendaji wa Benki ya NCBA kuanzia Julai 08, 2020 itakapoanza kutoa huduma zake rasmi.

Akithibitisha uteuzi wake, Mwenyekiti mteule wa bodi ya NCBA, Sharmapal Aggarwal alipongeza uteuzi wa Margaret wa kuteuliwa kwake.

 “Tunatambua uzoefu wake mkubwa kwenye sekta ya benki na tunasifu kwa kujitoa kwake upya kwenye benki. Tunaamini kuwa yeye ni mtu sahihi kuiongoza Benki ya NCBA kwenye zama mpya ya maendeleo endelevu na kuleta mafanikio kwa wadau wote Tanzania na bara la Afrika kwa ujumla,” alinukuliwa Aggarwal.

Vilevile alibainisha kuwa Gift Shoko ambaye ni Afisa Mkurugenzi Mkuu wa benki ya CBA Tanzania ndiye  mteule katika bodi ya benki ya NCBA kama Mtendaji Mkuu, na ameteuliwa kuiongoza taasisi mpya kama Mkurugenzi Mtendaji wa biashara za kidijitali na wateja wadogo na wakubwa.

Kwa mujibu wa Mwenyekiti huyo, nafasi ya Shoko itaiongoza benki ya NCBA kwenye biashara za kidijitali ambapo ni kiini cha ukuaji endelevu wa biashara ya kundi hili wakati inalenga kuwa benki inayoongoza kwenye kanda katika miaka mitano ijayo.

Kwa upande wake, Margaret ambaye ni Mkurugenzi Mkuu wa NIC Bank Tanzania akiwa ni mwenye uzoefu wa miaka 27 katika sekta ya benki alisema, “Huu ni ukurasa mpya kwa benki hizi mbili. Natazamia kufanya kazi na timu ya watu wenye nia moja ili kuimarisha taasisi yetu ya fedha nchini Tanzania.

“Taasisi hii mpya itaakisi dhamira na maadili kutoka benki zote mbili, baada ya kujifunza ubora wa pande zote na kujenga taasisi kubwa na bora ya kuwahudumia wateja na wadau wetu,” alinukuliwa mkurugenzi huyo.

Katika nyakati tofauti, Margaret amewahi kushikilia nyadhifa mbalimbali;  Mkurugenzi Mtendaji wa Mikopo Hatarishi kwenye NIC Bank Group nchini Kenya lakini pia amefanya kazi katika Benki ya Barclays Bank Kenya (kwa sasa ABSA Bank).

Kuhusu elimu ya Margaret, ana Shahada ya uzamili katika uratibu duniani (MBA ya Global Executive), Shahada ya Sayansi (BSc) na pia ana Stashahada ya usimamizi wa mahusiano ya wateja. Vilevile ni mwanachama wa Taasisi ya Masuala ya Kifedha, Kenya.

Naye Shoko ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa biashara za kidijitali alisema kuwa, “ Kuleta benki zote mbili pamoja imetuwezesha kukua na kuwa benki kubwa katika sekta ya digitali…

“… Kadri ambavyo teknolojia inaendelea kukua tunashuhudia teknolojia ikiwa inachukua nafasi muhimu zaidi katika kuleta ushirikishwaji wa kifedha nchini Tanzania, Afrika Mashariki na kwa bara zima kwa ujumla.  Tuna vifaa, rasilimali na wataalamu wa kutuwezesha kuongoza katika soko,” alisema Shoko. 

“Tumia teknolojia za kilimo na utawala bora kwa ukuaji wa ...

foto
Mwandishi: Alfred Lasteck

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi