loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

JPM ateua tena DC, wakurugenzi

RAIS John Magufuli amefanya uteuzi wa mkuu wa wilaya moja na wakurugenzi watendaji wa halmashauri mbalimbali ambao pamoja na wengine watatu walioteuliwa awali, wanatakiwa leo kuwapo Ikulu, Chamwino mkoani Dodoma .

Mkuu wa Wilaya aliyeteuliwa ni Albinus Mgonya ambaye anakuwa Mkuu wa Wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro. Kabla ya uteuzi huo, Mgonya alikuwa Katibu Tawala Msaidizi Mkoa wa Rukwa na anachukua nafasi ya Mohamed Utaly.

Halmashauri ambazo zimepata wakurugenzi watendaji wapya ni Newala, Halmashauri ya Mji wa Nanyamba, Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara na Halmashauri ya Wilaya ya Biharamulo. Nyingine ni Mvomero na Ifaraka za mkoani Morogoro.

Wakurugenzi hao ni Waziri Kombo anayekwenda Halmashauri ya Wilaya ya Biharamuro mkoani Kagera. Kabla ya uteuzi huo, Kombo alikuwa Ofisa Utumishi wa Manispaa ya Morogoro na anachukua nafasi ya Wendi Ng’ahala.

Wengine ni Duncan Thebas anayekwenda Newala ambaye kabla ya uteuzi alikuwa Ofisa Mipango wa Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa mkoani Dodoma.

Anachukua nafasi ya Mussa Chimae; Mwailafu Edwin aliyepangiwa Halmashauri ya Mji wa Nanyamba na kabla ya uteuzi alikuwa Ofisa Mipango wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi mkoani Singida anayechukua nafasi ya Oscar Ng’itu.

Aliyekuwa Katibu Tawala Msaidizi Mkoa wa Mbeya, Erica Yegella ameteuliwa kwenda Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara na amechukua nafasi ya Omari Kipanga. Mwingine ni Hassan Njama aliyeteuliwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero.

Kabla ya uteuzi, alikuwa Ofisa Mipango wa Halmashauri ya Mji wa Mtwara na anachukua nafasi ya Florent Kayombo.

Aliyekuwa Ofisa Mipango wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga mkoani Pwani, Kanyala Mahinda, ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mji wa Ifakara na kuchukua nafasi ya Francis Ndulane.

Awali, Rais alifanya uteuzi wa wakurugenzi watendaji watatu ambao pia wataungana na wateule wengine ikulu Chamwino.

Wateule hao ni Anastazia Tutuba anayekwenda Halmashauri ya Wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro. Wengine ni Saida Mutambule anayekwenda halmashauri ya wilaya ya Arusha na Elias Ng’wanidako anayekwenda kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa jiji la Mbeya.

MGOMBEA urais wa ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi

Magufuli: Nataka kumalizia kazi

masaa 3 yaliyopita Magnus Mahenge, Dodoma

MGOMBEA urais wa ...

Wanawake waihakikishia CCM ushindi

masaa 3 yaliyopita Magnus Mahenge, Dodoma

 

Waziri aagiza mifumo ya fedha ipunguze rushwa

masaa 5 yaliyopita Mwandishi Maalumu, Simiyu

WAZIRI ...